DISQUS SHORTNAME

MASKINI KICHANGA CHATUPWA MWANANYAMALA MAENEO YA MTO NGOMBE

MWILI wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na siku mbili umeokotwa ukiwa umetupwa eneo la mto Ng' ombe jirani na Rasco , Mwananyamala jiji...

MWILI wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na siku mbili umeokotwa ukiwa umetupwa eneo la mto Ng' ombe jirani na Rasco , Mwananyamala jijini Dar . Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo
kichanga hicho cha kiume kimekutwa eneo hilo leo asubuhi kikiwa kwenye mfuko wa Rambo .
Mtandao huu ulifanikiwa kuongea na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Bi . Husna aliyetoa rai kwa wananchi wa eneo lake kutojihusisha na vitendo viovu kama hiki , huku akiwasihi kutumia njia za uzazi wa mpango kujikinga na matatizo kama hayo. " Nina masikitiko makubwa kwa kitendo hiki , ni bora kichanga hiki kingeletwa serikalini tukilee kuliko kutupwa eneo hili . Kama wananchi mkishindwa kuvumilia bora mtumie
uzazi wa mpango," alisema Bi. Husna huku akiahidi kufanya uchunguzi wa kina kumtafuta muhusika !

Related

STORY ZA KITAA 2234016661153345851

Post a Comment

  1. jamani watu wana dhambi sana kwanini alibeba kama akijua hata zaa

    ReplyDelete
  2. RIP too sad by Sista duu wa kigoma ujiji

    ReplyDelete
  3. Binadam sis mungu atusamehe sna

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item