DISQUS SHORTNAME

WANAMUZIKI 5 TWANGA HOIKWA DENGUE

HOMA ya Dengue imezidi kuwa tishio jijini Dar es Salaam, ambapo wanamuziki watano wa Bendi ya African Stars ‘ Twanga Pepeta International...


HOMA ya Dengue imezidi kuwa tishio jijini Dar es Salaam, ambapo wanamuziki watano wa Bendi ya African Stars ‘ Twanga Pepeta International’ , wamekumbwa na ugonjwa huo, habari zimefika katika dawati la Risasi Mchanganyiko. Mmoja wa wanamuziki wa Twanga anayesumbuliwa na Homa ya Dengue , Bakari
Kasongo ‘ Mandela ’.

Mtoa habari Hassan Rehani ambaye ni meneja wa bendi hiyo , alizungumza na
mwandishi wetu hivi karibuni na kuwataja wanamuziki hao kuwa ni Badi Bakule , Ramadhan ‘ Pentagoni ’ , Bakari Kasongo ‘ Mandela ’ , Sabrina Mbetembete na Natalia Mbui. “Nimeshitushwa sana na ugonjwa huu,
maana katika maisha yangu ugonjwa ambao nilishawahi kuona unasumbua watu wa sehemu moja kwa wingi kiasi hiki ni Kipindupindu tu , sasa hii dengue ni hatari , ” alisema Rehani na kuongeza kuwa wanamuziki hao walikuwa wamelazwa Hospitali ya Mwananyamala na kwamba hali zao zilikuwa zinaendelea vizuri.
Naye mmoja wa wagonjwa hao , Rama Pentagoni, alipozungumza na mwandishi wetu alisema anaendelea vizuri, huku akiuelezea ugonjwa huo kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu.

Related

STORY ZA KITAA 8862651992697592189

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item