WEMA SEPETU NA MTITU KIMENUKA!
KIMENUKA ! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effects, William Mtitu wamekwidana ‘ live’ ndani ya gari...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/wema-sepetu-na-mtitu-kimenuka.html
KIMENUKA ! Beautiful Onyinye, Wema Isaac
Sepetu na Mkurugenzi wa Kampuni ya Five
Effects, William Mtitu wamekwidana ‘ live’
ndani ya gari , Risasi Jumamosi lina kisanga
kamili .
Staa katika tasnia ya filamu za Kibongo ,
Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu
UWANJA WA VITA
Taarifa za uhakika zilieleza kuwa , tukio hilo
lilijiri juzikati maeneo la Bunju , Dar nyumbani
kwa mke wa aliyekuwa mwigizaji na
prodyuza wa Bongo Movies , Adam Phillip
Kuambiana wakati ndugu , mastaa na jamaa
walipokuwa wameweka matanga ya msiba .
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoomba
kustiriwa gazetini, kisa cha yote kilidaiwa
kuwa ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity ,
Steven Mengere ‘ Steve Nyerere ’ kueneza
sumu kwa mastaa kuwa wawachunie Mtitu
na mwigizaji Jacob Steven ‘ JB ’ ambao
alitofautiana nao msibani hapo .
TUJIUNGE NA CHANZO
“Steve alipishana kauli na JB , Mtitu
akaingilia , sasa Steve akamwaga ‘ sumu ’ kwa
wasanii wengine ambao ghafla walianza
kuwachunia JB na Mtitu msibani hapo, ”
kilisema chanzo.
MTITI WAIBUKA
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa , Mtitu ,
baada ya kuchuniwa huko na wasanii
wengine, kuna wakati alikuwa kwenye gari na
kutaka kupishana na gari la mwigizaji Aunt
Ezekiel ambalo ndani yake alikuwemo Wema ,
mtiti ukaibuka.
“Aunt alishusha kioo na kumuuliza Mtitu
umemfanya nini Steve ? Wakati Mtitu akitaka
kumjibu juu ya kile kilichotokea , dada
mkubwa au mama la mama ( Wema )
akaununua ugomvi usiomhusu , ” kilitiririka
chanzo.
KIHEREHERE CHA WEMA CHAANZISHA
MTITI
Chanzo hicho bila kupepesa macho , kiliweka
bayana kuwa , Wema alindandia kauli ya Aunt
na kumwambia Mtitu ni mtu asiyempenda .
Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effects ,
William Mtitu akiweka shada la maua tatika
kabuli la kuambiana .
“Wema alisema katika watu ambao
hawapendi duniani , Mtitu ndiyo namba moja
ndipo hapo uvumilivu ulipomshinda Mtitu na
kushuka kwenda kumvaa Wema .
“Alipofika aliingiza mkono kupitia upenyo
mdogo ulioachwa katika dirisha , akafungua
loki ya mlango na kumkalia Wema mapajani
huku akimkwida shingoni.
“Wema naye akajibu mapigo kwa kumkwida
Mtitu huku akiporomosha maneno machafu
( hayaandikiki gazetini) ndipo Mtitu
alipoonesha uanaume na kumpa maneno ya
kuashiria atampa kipondo ambacho hajawahi
kukiona maishani mwake , ” kilisema chanzo.
AUNT AOKOA JAHAZI
Ilidaiwa kuwa , baada ya Wema kutaitiwa
vilivyo na Mtitu , Aunt ilibidi aingilie kati na
kumuomba Mtitu amsamehe bure na
amuondoe shetani eneo hilo.
“Aunt alimuomba sana Mtitu kuwa amuachie
Wema kwa kumsihi kuwa yeye
wanaheshimiana sana , Mtitu akamuachia na
kushuka ndani ya gari huku
akimtahadharisha Wema kuwa asije akarudia
kuingia kwenye kumi na nane zake, ” kilizidi
kumwaga data chanzo.
WAO WANASEMAJE ?
Baada ya kujiridhisha na chanzo hicho,
wanahabari wetu walianza kuwasaka
wahusika ambapo wa kwanza alikuwa ni
Wema ambaye simu yake iliita bila
kupokelewa ( anaweza kututafuta akiisoma
habari hii ) .
Baada ya Wema kutopokea , mapaparazi wetu
walimgeukia Mtitu ambaye alijibu kwa kifupi
kisha akakata simu na alipopigiwa tena ,
hakupokea:
“Mimi sipendi mambo ya kijinga , mtu hawezi
kuingilia visivyomhusu nikamuangalia tu .”
Jitihada za kumpata Aunt ziligonga mwamba
baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila
kupokelewa.
Source: Globel

Mdomo unaponza
ReplyDeleteMtitu huwa hanaga uswahili wala utoto, wema learn to behave, na tabia ya kupenda kutukana hovyo au kujifanya unahasira za mbogo itakuponza,,,,, angalia wasanii wenzio wakike ambao wanakusuport ni wangapi kama sio wachache sana, nakupenda mno lakini kwa hili hua unaniboaaaa endelea kua mzungu it wont cost u a thing mama, kuzungukwa na maadui si kuzuri hata kidogo
ReplyDelete