DISQUS SHORTNAME

AUNT EZEKIEL AWABWATUKIAWAKWE ZAKE

STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson Jujuman ameonesha upande wake wa pili baada ya kuwabwatukia wakwe zake aliposikia kuwa w...


STAA wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel
Grayson Jujuman ameonesha upande wake
wa pili baada ya kuwabwatukia wakwe zake
aliposikia kuwa wana mpango wa kumpa
talaka ili aachane na mumewe Sunday
Demonte kutokana na tabia yake kwa kuwa
siyo mwanamke wa kuoa ( wife material ) .
Staa wa sinema za Kibongo , Aunt Ezekiel
Grayson Jujuman .

Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati
jijini Dar , Aunt alidai kuwa alikerwa na jambo
hilo na kujikuta akishindwa kujizuia na
kuwawakia kuwa hajaolewa na ndugu hivyo
mwenye mamlaka ya kutoa talaka ni
mumewe pekee.
Aunt alisema kwamba , amekuwa akisikia
mara kwa mara habari za ndugu wa Demonte
wakiongea maneno mengi ya kumfitinisha na
mumewe.
Alidai naye ni binadamu hivyo jambo hilo
limekuwa likimkera kwa sababu wanaongea
maneno hayo pembeni na kwamba hakuna
hata mmoja aliyewahi kumfuata na
kumwambia juu ya suala hilo, zaidi amekuwa
akiambiwa na watu wengine tu .
Akifafanua zaidi , Aunt alisema kwamba
anawashangaa hao wanaojiita ndugu wa
Demonte kuendelea kumtolea maneno ya
kejeli kila kukicha na wakati kama wanahisi
kuna tatizo kati yake na mumewe wangeweza
kumtafuta na kuzungumza naye .
Aunt Ezekiel akiwa na mumewe Demonte
siku ya ndoa yao.
Alitiririka kuwa jambo ambalo halimpendezi
ni pale anapokutana na watu wakimtuhumu
kwamba eti ndugu wa mumewe wanataka
kumpatia talaka .
“Ujue hao ndugu wanaotaka kunipa talaka
wanatakiwa waelewe kuwa mimi sijaolewa na
wao , hivyo hata jukumu la kunipa talaka siyo
lao, maana niko vizuri na mume wangu, wala
hatujawahi kukwaruzana hata kuambiana
ishu za kupeana talaka , ” alisema Aunt.
Ndoa ya Aunt imekuwa ikisengenywa tangu
ilipofungwa mwezi June , 2012 kufutia staa
huyo kutoishi pamoja na mumewe ambaye
inasemekana anaishi Dubai.

Related

BONGO MOVIE 2992031450169075204

Post a Comment

  1. Kama aliolewa kiislamu ajue kuwa ndugu wa damu wa mumewe wanaweza kumpa talaka ata wakwe pia wanaweza kumpa talaka n ikaswihi as long as mumewe karidhia kumuacha coz karatasi ni ushahidi2 talaka ni maneno n imani ya mume kumuacha mke......
    Im out

    ReplyDelete
  2. Mbona uyo ni mtoto kama,, au ndo mumewe

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item