LULU AKACHA MSIBA WAKUAMBIANA , AJITETEA
STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘ Lulu’ amedaiwa kuukacha msiba wa aliyekuwa nguli wa filamu za Kibongo, Adam Philip Kuambi...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/lulu-akacha-msiba-wa-kuambiana-ajitetea.html
STAA wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘ Lulu’ amedaiwa kuukacha msiba wa
aliyekuwa nguli wa filamu za Kibongo, Adam
Philip Kuambiana na kujitetea kuwa alibanwa
na majukumu .
Alipobanwa na mwanahabari wetu kuhusu
kutohudhuria msiba huo uliodumu kwa
takriban siku nne, Lulu alijitetea kuwa
alikuwa Mwanza kikazi .
Elizabeth Michael ‘Lulu ’ .
“Nimebanwa na kazi , nipo Mwanza na
kampuni yetu tunayofanya nayo kazi imetoa
nafasi moja tu kurudi Dar kwenye msiba,
nimeshindwa , ” alisema Lulu.
Mastaa wengi walijitokeza kwenye msiba huo
akiwemo Jacob Steven ‘ JB ’ ambaye alikuwa
nchini Uturuki kikazi lakini akaziacha na
kurejea Bongo kumpumzisha prodyuza wake .
