DISQUS SHORTNAME

HUYU NDO MBIBIALIYEKAMATWA NA MADAWA YAKULEVYA UWANJA WA JKNYERERE

Dar es Salaam. Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulev...


Dar es Salaam. Bibi mmoja raia wa Nigeria,
Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja rekodi ya umri
wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za
kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA).
Cole alikamatwa Jumatatu akiwa amemeza kete
82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa
kwenye karatasi zinazofanana na ganda la
sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika
mitambo.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu
wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za
Kulevya, Alfred Nzowa zimesema pamoja na
mbinu zake na kujiamini, mwanamke huyo
alikamatwa kutokana na ushirikiano wa vitengo
mbalimbali vya uwanja wa ndege.
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege,
Hamisi Selemani alisema mwanamke huyo
alikamatwa Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri
akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya
Shirika la Ndege la Ethiopia.
Selemani alisema raia huyo aliwasili nchini Mei
15, mwaka huu na alikaa muda wote bila ya
kuwa na shughuli yoyote, jambo ambalo lilitiliwa
shaka na kumkamata.
“Huyu mwanamke achana naye, akisimama
mbele yako huwezi ukaamini kwa jinsi
anavyojiamini. Alikuwa na mbinu mpya ya
kufunga hizo kete. Kila moja ilifungwa kwa
karatasi inayofanana na ganda la sigara,”
alisema Selemani.
Alisema mwanamke huyo alitumia mbinu hiyo ili
asigundulike wakati akikaguliwa kwa mitambo
maalumu inayogundua dawa za kulevya.
Taarifa zaidi zinasema kuwa kutokana na mbinu
yake ya ufungaji wa kete, mwanamke huyo
alikuwa tayari amevuka hatua ya kwanza ya
ukaguzi.
Nzowa alisema baada ya kumhoji, mtuhumiwa
huyo alidai kuwa aliingia nchini kwa ajili ya
kutafuta soko la kuuza vipodozi na nguo.
“Wakati tukiendelea kumhoji, Kikosi Kazi cha
Kuthibiti Dawa za Kulevya kilibaini na kugundua
kuwa alikuwa amemeza dawa za kulevya.
“Huyu ni mzee, lakini tumeshangaa kuona bado
ana nguvu za kutosha na tulishangaa baada ya
kutoa kete 20 kwa mara moja katika awamu ya
kwanza, jambo hili si rahisi kutokana na umri
wake,” alisema Nzowa.
Mtuhumiwa huyo aliyekuwa na hati ya kusafiria
ya Nigeria, anaendelea kuhojiwa na upelelezi
ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Related

HABARI YA MJINI 1724285157037641345

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item