WAPAMBE WAMFUATA VICKY KAMATA WODINI WAKIWA WAMETINGA SARE ZAO ZA HARUSI
MAMBO yanazidi kuwa mambo kuhusu ile ndoa ya Mbunge Vicky Kamata iliyoyeyuka katika dakika za majeruhi , safari hii Risasi Mchanganyiko ...
MAMBO yanazidi kuwa mambo kuhusu ile
ndoa ya Mbunge Vicky Kamata iliyoyeyuka
katika dakika za majeruhi , safari hii Risasi
Mchanganyiko limefanikiwa kuwanasa baadhi
ya wapambe ambao walitakiwa kuwa kwenye
msafara wa harusi hiyo kutoka kanisani hadi
ukumbini.
Baadhi ya wapambe waliotakiwa kuwepo
katika harusi ya Vicky Kamata
walipomtembelea wodini
Wapambe hao walitia timu kwenye wodi
aliyokuwa amelazwa Vicky katika Hospitali
ya General iliyopo Tabata jijini Dar es
Salaam, Jumamosi iliyopita ( ambayo ndiyo
ilikuwa ndoa ifungwe ) .
WAPAMBE WATATU
Katika idadi ya watu sita waliofika kumjulia
hali Vicky , watatu wakiwemo wanaume wawili
ndiyo waliokuwa wamevaa sare ya harusi
hiyo ambayo ingetawaliwa na rangi ya purple
‘ papo ’
SARE KAMILI
Iilithibitika kwamba sare za shughuli hiyo
zilishashonwa, wanaume waliokuwa mstari
wa kusindikiza maharusi walitakiwa kuvaa
suti nyeusi ( single button ) , shati jeupe na tai
fupi ( necktie ) yenye rangi ya papo .
Wapambe wakiwa wodini kumfariji Vicky .
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wanawake
ambao pia walikuwa kwenye msafara wa
maharusi ( ma - maids) walitakiwa kuvaa
magauni ya rangi hiyohiyo ya papo .
KWA NINI WALIVAA HUKU WAKIJUA
HARUSI HAIPO ?
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wapambe hao
walikuwa ndani ya mavazi hayo kwa sababu
walijua baada ya ndoa kuyeyuka ,
wasingeweza kuvaa siku nyingine .
“Unajua wale si kwamba walikwenda pale na
sare wakijua ndoa ipo, walijua kabisa
kwamba haipo ila sasa kwa sababu ndiyo
ilikuwa siku yenyewe ilibidi wajipigilie tu
kama kusafisha hali ya hewa au wengine
husema ‘ kuoshea ’ jina, ” kilisema chanzo.
UKUMBI WADODA
Waandishi wetu Jumapili iliyopita walikwenda
mbele zaidi kwa kufika kwenye Hoteli ya
Hyatt Regency The Kilimanjaro ya jijini Dar es
Salaam ambako shughuli ya ndoa hiyo
ingefanyikia .
Mfanyakazi mmoja ambaye aligoma kutaja
jina kwa sababu si msemaji wa hoteli hiyo
alisema ukumbi ambao ulikuwa utumike kwa
harusi ya Vicky Kamata uitwao Kili Marquee
ulilala doro baada ya wahusika kuweka wazi
kwamba hakuna harusi tena .
“Ukumbi ulilala mtupu , taarifa zilishakuja
mapema kwamba hakuna harusi , ” alisema
mfanyakazi huyo .
Alipoulizwa ni kwa nini wasikodishe kwa mtu
mwingine , mfanyakazi huyo alisema si
utaratibu wa hoteli hiyo .
“Wale walishalipia , sasa ukisema ukodishe
kwa wengine kwa sababu harusi haipo , je ,
ingetokea harusi ikaja ghafla na kukuta
wateja wengine ? Si ingekula kwetu ?” Alisema
mfanyakazi huyo .
MILIONI 40 ZA MCHANGO ZATATIZA
Kuna habari kwamba, zaidi ya shilingi milioni
arobaini ambazo zilikuwa za mchango wa
harusi hiyo zimetoweka kusikojulikana .
Fedha hizo zilichangwa na wadau mbalimbali
katika kufikia kile kiasi cha shilingi milioni 96
ambazo zilidaiwa tangu awali kwamba ndizo
zingefanikisha shughuli nzima ya harusi hiyo
iliyotarajiwa kuwa ya kifahari .
Vicky Kamata akiwa katika pozi na
mwanaume aliyepanga kuoana naye
anayejulikana kwa jina la Charles ambaye
kwa sasa hajulikani alipo .
BWANA HARUSI HAJULIKANI ALIPO
Ili kupata uwiano sawa wa habari hii , juzi
Jumatatu waandishi wetu walimtafuta
mwanaume aliyetarajiwa kufunga ndoa na
Vicky , Charles kwenye ofisi ya kampuni moja
ya simu za mkononi , Kijitonyama jijini Dar
lakini baadhi ya wafanyakazi walisema ana
wiki mbili hajakanyaga kazini .
“Huyu bosi hajakanyaga hapa wiki mbili,
hayupo, ” alijibu mfanyakazi mmoja .
Risasi Mchanganyiko : “Hajakanyaga kivipi?
Kasafiri, yuko likizo au ?”
Mfanyakazi: “Aliandika barua ya kuomba
mapumziko ya wiki mbili kwa hiyo hatujui
yuko wapi kwa sasa . ”
Vicky Kamata akiendelea kupata matibabu
katika Hospitali ya Tabata General jijini Dar .
NYUMBANI KWA VICKY
Baada ya kutoka ofisini kwa bwana harusi ,
wanahabari wetu walitinga nyumbani kwa
bibi harusi Vicky Kamata , Sinza ya Vatican,
Dar na kukumbana na mlinzi getini ambaye
alisema mgonjwa huyo aliruhusiwa kutoka
hospitali saa mbili usiku wa Jumapili lakini
alikuwa amelala na haruhusiwi kuzungumza
na mtu yeyote zaidi ya kupumzika.
“Mheshimiwa karudi jana usiku saa mbili
lakini haruhusiwi kuzungumza na watu ,
amelala, ” alisema mlinzi huyo.
