Huyu ndio jamaa ambaye kampa mwanae jina la Yesu ingawa kanisa limekataa kumbatiza mtoto huyo.
Ndiritu Njoka kwenye headlines tena wakati huu sio kukabiliana na wanawake wanao wapiga waume zao wakati huu jamaa anataka kanisa na Pres...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/huyu-ndio-jamaa-ambaye-kampa-mwane-jina.html
Ndiritu Njoka kwenye headlines tena wakati huu sio kukabiliana na wanawake wanao wapiga waume zao wakati huu jamaa anataka kanisa na Presibiteria ya Africa Mashariki- PCEA kumbatiza mwanae wa kiume jina la Jesus ama yesu.
Njoka amesema ameamua kumpa mwanae jina hilo kwasababu jina Yesu ni jina zuri
sana>>’Sijamuita mwanangu kristo,nimemuita Yesu kwasababu ni jina nzuri sana’ Njoka pia amedai kwamba kanisa na hata hospitali aliyozaliwa mwanae wamekataa kumuandikia cheti cha taarifa ya kuzaliwa kwasababu hawataki kuandika Jina Yesu kwenye cheti hicho. Njoka alipoulizwa kuhusu hilo amesema >>’hata kama hospitali walikataa kuandika hilo jina Yesu, nitatumia mkono wangu kuandika hiyo
taarifa ya kuzaliwa Yesu Njoka Njoka, kwasababu huyo ni mwanangu’. Rais huyo wa Wanaume aliyejitangaza ameongeza kuwa ameacha kwenda kanisani kwasababu ya wao kukataa mwanawe kuitwa yesu>’nimewaambia sawa basi,hata hayo mambo ya kanisa nitaacha na ni nitakua nikiomba nyumbani kwasababu kama shida ni kumwita mwanangu yesu si lazima niende kanisani’ Nae katibu mkuu wa kanisa hilo la PCEA Kasisi Thegu Mutahi anasema kwamba jina la yesu hawezi kupewa mtu maana yesu ni mwana wa mungu>’ukimuita mtoto yesu unamwona hapo barabarani akicheza na wenzake anaitwa Yesu !, Yesu !, Yesu ! hilo jina na tunajua yesu ni mwokozi litachukuliwa hivi hivi’. Aidha njoka amesema amekerwa na hatua ya kanisa kukataa majina mazuri wakati wananyamaza watu wanaojiita Mwashetani na wengine Mwakaburi,kwa sasa Njoka amesema kwamba amemuandikia barua Papa Francis Benedict XVI kama njia ya kutafuta kibali kumuita mwanae Yesu Njoka Njoka.

