Steve Nyerere achaguliwa kuwamwenyekiti wa wasanii upande waAmani nje ya Bunge la katiba
Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amechaguliwa na Kamati ya Tanzania kwanza kuwa mwenyekiti wa wasanii wa amani ndani ya Tanzania nj...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/steve-nyerere-achaguliwa-kuwa.html
Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere
amechaguliwa na Kamati ya Tanzania kwanza
kuwa mwenyekiti wa wasanii wa amani ndani ya
Tanzania nje ya Bunge la katiba.
Akizungumza na Bongo5, Steve Nyerere amesema
amechaguliwa na Kamati ya Tanzania Kwanza nje
ya Bunge kwa lengo la kuhamasisha Amani kwa
wananchi wa Tanzania.
“Walikaa kamati zao hapa Dar es salaam
wakakaa Zanzibar na kura zote walizopiga
zilimdondokea Steve Nyerere, mwenyekiti wa
wasanii upande wa Amani nje ya Bunge la Katiba.
Baada ya hapo nilipigiwa simu ambapo nikiwa
sijui lolote nilikuta kwanza barua nyumbani
kwamba nahitajika kwenye kikao,nikasema ni
jambo zuri, mimi naimani bila amani na mimi
nilitoa ufafanuzi wangu bila amani hata kazi
zangu haziwezi kwenda. Nahitaji amani sana ili
ziweze kwenda. Lakini nikasema hata wasanii bila
kujali hela ya malipo, haya malipo yanakuja nchi
ikiwa na amani na utulivu.Tunaona wasanii wa
nchi mbalimbali duniani wanapigania amani ya za
nchi zao. Kwanini sisi tushindwe,kwanini
JB,Diamond,Lady Jaydee na wasanii wengine
wasiwe mabalozi wa amani nchini? Tukijipanga
tunaweza,” amesema.
“Lakini vilevile nilichokipenda mimi nimepewa
jukumu nichague wasanii wenzangu ambao
wanaweza wakaitangaza amani ndani ya nchi na
nje ya nchi yetu. Wapo wengi wenye uwezo
kwenye ma group yote ya wasani,wapo wa
filamu,muziki,ngoma za asili kote huko inabidi
tupate mabalozi kumi ambao wataweza kufanya
kazi kwa ukamilifu zaidi. Kwahiyo hili ni suala
langu nadhani nikikaa chini nitajua nani anafaa
na nani hafai.”

Hongera mwenyekiti
ReplyDelete