Dina Marious wa Clouds FMkutofanya tena kipindi cha ‘LeoTena’, akabidhiwa show mpya yaTV
Mtangazaji wa kipindi cha ‘Leo Tena’ cha Clouds Fm, Dina Marious leo ametangaza kuwa hataendelea kufanya kipindi hicho na badala yake an...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/dina-marious-wa-clouds-fm-kutofanya.html
Mtangazaji wa kipindi cha ‘Leo Tena’ cha Clouds
Fm, Dina Marious leo ametangaza kuwa
hataendelea kufanya kipindi hicho na badala yake
anakuja na kipindi kipya cha TV.
Dina ambaye hajasikika kwenye kipindi hicho kwa
miezi kadhaa baada ya kwenda likizo ya uzazi
baada ya kujifungua mtoto wa kiume aitwaye
Zion, ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake ya
Instagram.
Hiki ndicho alichokiandika:
“Ni miaka 8 sasa imetimia toka nilipokabidhiwa
mtoto huyo.Nilimlea kwa taabu sana siku za
mwanzo zilikiwa ngumu wakati mwingine sikulala
kuhakikisha anakuwa salama. Nyakati hizo
nilionekana nisingekuwa mama bora wa mtoto
huyo lakini nilipigana kike na kuwa mtoto bora
aliyependwa na kusifika nchi nzima.Mtoto huyo
anaitwa leo tena na Dina Marios.
Leo tena ikawa leo tena na kuwa kipindi bora
kinachopendwa tanzania na dina marios nikawa
mtangazaji bora wa kike na wapili bora Tz nzima
kwa kupendwa hii ni kwa mujimu wa
research.Kupitia leo tena nimetengeneza
mashabiki,marafiki,wapenzi,na hata ndugu.Sasa
leo tena imekuwa na sina budi kuiacha iendelee
kulelewa na mtu mwingine.
Kama nilivyokabidhiwa leo tena kuilea nimepewa
tena jukumu lingine kubwa la kulea mtoto mpya
atakaeonekana kwenye luninga inamaana
ntakuwa nikiuza sura luningani.Niliwapenda sana
wasikilizaji wangu japo mlikuwa mkiniuliza
narejea lini kwenye leo tena ukweli ni kwamba
sirudi tena kwenye leo tena.
Naomba sala na dua zenu katika safari yangu
mpya ambayo najua haitakuwa rahisi kama
mlivyokuwa nami kwenye leo tena basi muwe
nami katika hili.Wiki ijayo nitakuja rasmi kuwaaga
kupitia leo tena ya clouds fm.Nawapenda mno
*machozi kede kede yananimwagika*”
