Feza asimulia maisha ya South,adai alihama chuo alichokuwaakisoma kutokana na watukumshangaa
Mshiriki wa Big Brother Afrika, 2013 Feza Kessy ameelezea maisha yake baada ya kuhamia nchini Afrika Kusini atikokea nchini Botswana kwa ...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/feza-asimulia-maisha-ya-south-adai.html
Mshiriki wa Big Brother Afrika, 2013 Feza Kessy
ameelezea maisha yake baada ya kuhamia nchini
Afrika Kusini atikokea nchini Botswana kwa
mpenzi wake O’neal aliyekuwa mshiriki mwenzake
wa BBA.
Feza ambaye kwa sasa yupo jijini Arusha
kusalimia ndugu zake,ameimbia 255 ya XXL ndani
ya Clouds FM kuwa amejikuta akipata mashabiki
wengi nchini Afrika kusini baada kuhamia.
“Sipo Botswana, sasa naishi South Africa
nasoma, nafanya part recording. Kwahiyo najaribu
kupita kwenye industry kule ya muziki,ipo slow
kidogo kwangu mimi kwasababu ni Mtanzania
obvious. Kwahiyo kuna mambo mengi najifunza.
Lakini nasoma and najaribu kurekodi kule,
nasomea Community Development. It’s
something kipo kwenye my heart. I think ni
something ambacho kitanisaidia itasaidia pia
jamii yangu. Nilienda chuo cha kwanza
nikashindwa kuendelea kwasababu ilikuwa ni
vurugu pale nilabidi nihamie kwenye college
ndogo ambayo ina watu wachache kwasababu
kule mpaka sasa hivi sio kama bongo watu just
wakikuona wanakushangaa wanakuomba
autograph kwahiyo ikawa nimelose focus. So
sasa hivi ni kwenye kingine sipendi kutaja taja.
Siku aa kabisa yani siku mbili nikaona hali
inaendelea vilevile watu kuja kushangaa hata
sikujua wame nirecognize vipi. Kwahiyo nikaona
‘heeh hata walimu pia ilikuwa inaleta kama kama
kero fulani,” amesema.
Kuhusu album yake, Feza amesema|:
“Natarajia album yangu itoke mwishoni mwa
mwaka huu. So mimi ni Mtanzania nataka ni
represent Tanzania lakini at the same time Africa
nzima inanitambua sasa hivi na hii ni opportunity
nzuri ya kuutoa muziki wa Tanzania nje ili
ujulikane. So for me najaribu kubalance Tanzania,
Kenya,Uganda ,West Africa na South Afrika. Kwa
sasa hivi nafanya kazi mwenyewe. Na yeye
(O’neal) yupo South Africa anaanza kazi very
soon huko huko Afrika Kusini kwenye radio, ni
radio presenter.”
