Picha: Mrembo huyu maarufu atakuwepo kwenye show ya Road2MAMA, Bilicanas, Ijumaa hii
Umezoea kumuona akitangaza vipindi mbalimbali kupitia kituo cha MTV Base, na sasa huenda ukawa mwenye bahati ya kumuona Nomuzi Mabena a...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/picha-mrembo-huyu-maarufu-atakuwepo.html
Umezoea kumuona akitangaza vipindi mbalimbali kupitia kituo cha MTV Base, na sasa huenda ukawa mwenye bahati ya kumuona Nomuzi Mabena akifanya yake live bila chenga Ijumaa hii kwenye ukumbi wa Club Bilicanas pale kituo hicho kitakapoangusha party ya mwaka ya Road to MAMA.
Nomuzi Mabena Pamoja na kumuona mrembo huyo, show hiyo ya kupigia debe tuzo za MAMA zitakazofanyika mwezi ujao nchini Afrika Kusini, wasanii kama Professor wa Afrika Kusini, Radio na Weasel, Sauti Sol na Diamond watatumbuiza. Pia DJ Tira wa Afrika Kusini atadondosha ngoma akishirikiana na madj wa nyumbani, Stevie B, Mafuvu na Zero. Usikose.

