MCHUMBA WA KUAMBIANAAIBUKA!
MAMBO yameanza! Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibu...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/mchumba-wa-kuambiana-aibuka.html
MAMBO yameanza! Siku mbili tu baada ya mazishi ya mwigizaji na mwongoza filamu mahiri Bongo, marehemu Adam Kuambiana, mrembo mmoja ameibuka na kusema alikuwa mchumba wa marehemu, Ijumaa linakujuza . Mrembo anayejulikana kwa jina la Lulu Jumanne ‘Selina’ . Kwa mujibu wa mrembo huyo, Lulu Jumanne ‘ Selina’ , alifahamiana na marehemu Kuambiana mwaka 2006 akamwambia ndoa
yake haipo sawasawa. Alisema walianzisha uhusiano lakini haukuwa wazi katika jamii . Alisema siku moja akiwa anaishi Mwananyamala , wazazi wake walimtembelea.
“Nikiwa na wazazi nilimwona Kuambiana anapiga hodi, akaingia akiwa na begi la nguo. Niliogopa kwani wazazi walikuwepo na walikuwa hawamtambui . Lulu Jumanne ‘Selina’ , akiwa na marehemu Kuambiana . “Hata hivyo , walielewa yakapita , tukawa tunaishi wote nyumbani kwa kupika na kupakua, ” alisema Selina ambaye naye ni mwigizaji. Aliendelea kuweka wazi kwamba, baada ya hao maisha yaliendelea lakini ikafika mahali
marehemu akahamishia mapenzi kwa Mbongo Fleva , Stara Thomas yeye akawa ‘ zilipendwa’ .
Akizidi kuanika mambo kuwa mwaka jana Kuambiana alirudi kwake baada ya kutofautiana na Stara, akataka waendelee na mapenzi yao. Katika mahojiano mafupi kati ya Selina na azeti hili , mambo yalikuwa hivi :
Ijumaa : Mlikuwa na mipango gani ya maisha?
Selina: Mingi tu . Kwanza alishanitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake na wadogo zake.
Ijumaa : Marehemu alionesha upendo wa dhati kwako ?
Selina: Sana tu , kwani alipenda kuniita mke wake. Alikuwa ananiheshimu hadi mwisho .Hakuwa akipenda mwanaume anizoee .
Ijumaa : Unajua nini kuhusu kuumwa kwake?
Selina: Najua alikuwa anaumwa tumbo kwa muda mrefu. Alikuwa akila chakula cha maelekezo ya daktari .
Ijumaa : Mara ya mwisho ulizungumza naye nini?
Selina: Nilimshauri anunue simu yenye WhatsApp kwani mara nyingi Kuambiana alikuwa hapatikani hewani . Alikuwa hawezi kukaa na simu kwa muda mrefu. Hata hivyo , Selina alisema hapendi kueleza mengi lakini anaamini yeye ndiye mwanamke wa mwisho katika mapenzi na marehemu .

