MAIMARTHA AWAUZIA MASTAADAWA ZA KUKUZA MAKALIO
MTANGAZAJI aliyepata kuwika katika vituo mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha Jesse, amedaiwa kuwauzia mastaa wa mjini dawa za kuonge...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/maimartha-awauzia-mastaa-dawa-za-kukuza.html
MTANGAZAJI aliyepata kuwika katika vituo
mbalimbali vya runinga Bongo, Maimartha
Jesse, amedaiwa kuwauzia mastaa wa mjini
dawa za kuongeza makalio.Habari za moto
kutoka kwa sosi wa kuaminika, zinasema
kuwa Maimartha ambaye pia huitwa Mai
amefikia hatua hiyo baada ya yeye kutumia
na kufanikiwa .
Mtangazaji aliyepata kuwika katika vituo
mbalimbali vya runinga Bongo , Maimartha
Jesse.
“Hamshangai siku hizi kila staa anaonekana
kuwa na makalio makubwa? Ni kazi ya Mai
hiyo . Anafanya hiyo biashara muda mrefu
sana. Ni za kunywa na kupaka.
“Mbona hata yeye ametumia dawa hizo muda
mrefu sana? Ukimwangalia utagundua
zamani hakuwa na hipsi za kiivyo. Ni kwa
sababu ya dawa, ” alisema sosi huyo.
Akaongeza: “Hata Lulu Semagongo ( Aunt
Lulu) ndiye aliyemsababishia kuwa na
makalio makubwa kwani wakati wako karibu
alikuwa akimpa dawa hizo .”
Waandishi wetu walifika dukani kwa Mai bila
kujua kama ni waandishi na kuulizia bidhaa
hizo ambapo zilitolewa , wakapiga picha bila
kugundulika.
Mai akiwa hajui kuwa yupo mikononi mwa
mapaparazi waliokuwa na njaa ya habari,
aliwaambia: “Ni dawa nzuri , mara moja
zinarekebisha umbo na unakuwa wa kuvutia.
Kuna za shilingi 250, 000 na 260, 000
inategemea kama ni vidonge au losheni .”
Mapaparazi wetu walipompigia simu Mai
baada ya kutoka dukani hapo na kumweleza
kuhusu uuzaji wa dawa hizo dukani kwake,
alisema duka lake linauza urembo wa aina
zote kwa mastaa na wasio mastaa.
“Kama nimetumia dawa za kuongeza
makalio, nyie inawahusu nini? Kifupi duka
langu linadili na urembo wa aina zote, ”
alisema Mai akishindwa kufafanua zaidi .
Lulu alipovutiwa waya na kuulizwa kama
makalio yake ni matokeo mazuri ya dawa za
Mai alisema : “Sijawahi kutumia dawa za Mai
kwa ajili ya kuongeza makalio.
Yangu ya asili lakini watu wakinipigia simu
na kuniuliza dawa za kuongeza makalio huwa
nawaelekeza kwa Mai .”

wapi hilo duka mwanamke makalio babu ee
ReplyDelete