DISQUS SHORTNAME

WEMA ALIONYWA VYA RAFIKI YAKE KUMSALITI ONA ALIVYOJIBU

FUATILIA MAHOJIANO YA WEMA NA BONGO 5 MIEZI 5 ILIYOPITA ILIKUA SIKU YA KUZALIWA KWAKE YAANI BIRTHDAY YAKE: Naomba nikukumbushe kw...

FUATILIA MAHOJIANO YA WEMA NA BONGO 5 MIEZI 5 ILIYOPITA ILIKUA SIKU YA KUZALIWA KWAKE YAANI BIRTHDAY YAKE:

Naomba nikukumbushe kwa ufupi namna Wema alivymeet na Diamond na Usaliti ulivyoanza na alijibu nini kila aliposalitiwa na rafiki zake wa karibu;

Hebu tuzungumzie uhusiano wako na Diamond ambao katika mahusiano yako yote ndio ulioandikwa zaidi kwenye magazeti, unakumbuka mlikutana wapi?

Mi na Diamond tuliwahi kukutana mara moja tu Billcanaz na hatukuwahi kusalimiana kabla ya kuanza uhusiano lakini tulikuwa tunaangalia sana, so nakumbuka alikuwa yupo smoking room kwahiyo tukawa tumepeana migongo, nilikuwa na rafiki zangu wawili. Nikamuona akaniona yeye alikuwa na rafiki yake, hatujasaliamija hatujafanya chochote mimi nimechukua vinywaji tukatoka nje na marafiki zangu tumesimama hapo nje nikawa naambiwa ‘yule ndio ameimba Kamwambie’ kipindi hicho nilikuwa namuona wa ajabu sana ila tu alijiseksisha kiasi fulani (kicheko kirefu).

Kipindi hicho mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba so nakumbuka hiyo ndio ilikuwa the first and last day tumeonana. Mimi nikasafiri nikaenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndio ilikuwa hot na Mbagala ndio karelease. Dada zangu walikuwa wanampenda sana Diamond yaani just from the songs. Dada yangu wa kwanza ana miaka 14 yupo Marekani na hajawahi kurudi Bongo toka aondoke kwahiyo alikuwa anaona Bongo inafanya vizuri sasa hivi akaniuliza kama tuna urafiki na Diamond nikasema sio sana tunajuana tu. 
Akaniambia nimwambia aende Marekani kufanya show sababu kila party tuliyokuwa tunaenda lazima watapiga Kamwambie halafu kila mtu anaipenda. So watu wakaanza kuniambia like ‘hebu find contact naye huku kuna mapromoter aje kufanya show’na kipindi hicho Profesa ndio alikuwa amekuja nikamwambia basi sawa mi nitamtafuta.

Nikamwabia Da Rehema, Ray C anitafutie contact zake. So siku moja nikaona anaplan kwenda kufanya show London, nika mclick Diamond Platnumz nikamtext, nikamwambia ‘hey mambo vp mzima upo London’ akaniambia ‘No mamie sipo London sijui ni nini’ nikamwabia ‘anyways Wema hapa nipo Marekani halafu it happens una fans wengi, akaniambia basi sawa acha nimalize issue ya London halafu nitakuambia. 
Basi tukajenga tu mazoea tukawa tunachat nini yaani ikawa yeye anaingia Facebook kuchat na mimi naingia kuchat naye, washkaji tu yaani. Akawa ananiambia ‘bado uko na Chaz na nini’ nikamwambia yeah nipo na Chaz. Sasa ilikuwa ni kama mwezi wa nane wa tisa kama sikosei. Mimi wakati nipo Marekani nilikuwa naambiwa sana news kuhusu Chaz, mara Chaz sijui yupo na mwanamke gani, hiyo hiyo Facebook watu wananitumia mpaka picha nikumuuliza anakataa.

Sasa mimi nakumbuka dada yangu alikuwa anampenda sana Chaz so siku ya siku amekutana naye yupo sijui na mwanamke gani alipoaniambia nikasema, basi. So nikajikuta namuelezea matatizo Diamond. Siku niliyoamua kabisa mimi and Chaz are done nikamwambia mimi siwezi. So tukawa tunawasiliana na Naseeb hivyo. Siku moja tukanuniana, alikuwa amealikwa Ikulu halafu nikawa namtext hajibu, nikimpigia simu hapokei akaja akatoka akanipigia simu nikawa sijibu. Akanitumia meseji ‘baby I am sorry, we ndio faraja yangu sijui ni nini…. I LOVE YOU. Sikuona kitu kingine chochote nikaona tu hiyo. Basi nami nikamjibu sawa nimekusamehe lakini sijakusamehe sana, nimekusame kidogo. Akaniambia ‘niambie kitu kizuri’ na mimi nikamwambia I LOVE YOU. Basi akaniambia ‘mwenzio nakupenda, nachanganyikiwa’ basi no mapenzi yakaanza hapo.So niliporudi kutoka Marekani mimi na Naseeb tukaanza kuishi pamoja. 

RAFIKI YAKE PENNY ANAMGEUKA

Penny alikuwa rafiki yaki tangu utotoni, unahisi alikuzunguka kwa Diamond?

It’s a free world, kila mmoja ana uhuru wake wa kuishi anavyotaka yeye. They met, they fall in love wameanza mapenzi, mtu yoyote anaweza kufall in love na mtu yeyote asiwe questioned. Love doesn’t ask why, haiulizi kwanini, because alikuwa rafiki yangu then I can’t NO. Wapendana, I wish them all the best. Mimi na Penny si kwamba hatuongei sio sababu ya hii issue, tuna drama zetu tu za huko nyuma kwahiyo hii issue ni muendelezo tu.

ALIONYWA KUHUSU KAJALA NA AKAPINGA KUA KAJALA HAWEZI KUMGEUKA

KUSIKILIZA WANACHOSEMA WATU MDA MWINGINE HUSAIDIA KUEPUSHA MAMBO MENGI TUNACHOPENDA KUSEMA NI KWAMBA WEMA KATUMIA BUSARA KUKAA KIMYA NA KUREALIZE KUA RAFIKI YAKE SI MZURI LAKINI PIA SI MARA YA KWANZA ANAGEUKWA NA RAFIKI YAKE HAPO JUU PIA TUMEONA PENNY ALIFANYA KITU HICHO HICHO WANAUME ARE SO MOVED AND TEMPED KIRAHISI HASA ANAPOKUA MAZINGIRA HATARISHI HATUSEMI DIAMOND NI MDHAIFU LA...TUNAMAANISHA WANAUME WOTE "NO HEROES INFRONT OF WOMEN" NI KUA MAKINI NA KUMWEKEA MWENZIO MIPAKA KATI YAKE NA MASHOGA ZAKO LAKINI PIA KAJALA NAE AJIREKEBISHE HII TABIA ALIYONAYO SI NZURI NA SASA HIVI  NI MAMA UNATEGEMEA MWANAO ANAJIFUNZA NINI KAMA ATAONA NA KUSOMA MAMBO UNAYOFANYA ??? NATUMAINI KISWAHILI KINAELEWEKA VIZURI JAMANI NA ATAKUA KASOMA COMMENTS ZENU NA USHAURI,KAZI KWAKE

Related

ZA MOTO 8718461118998518683

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item