DISQUS SHORTNAME

Master J KIKAANGONI LIVE: PRODYUZA WA DIAMOND ALISTAHILI TUZO,MAN WATER HAKUSTAHILI,AZUNGUMZIA NDOA YAKE NA SHAA

Producer mkongwe Joachim Kimaryo aka Master J ametoa mtazamo wake kuhusu tuzo za KTMA 2014 ambao unaonesha hakuridhishwa na mshindi wa tu...


Producer mkongwe Joachim Kimaryo aka Master J ametoa mtazamo wake kuhusu tuzo za KTMA 2014 ambao unaonesha hakuridhishwa na mshindi wa tuzo ya mtayarishaji bora wa mwaka – kizazi kipya ambaye ni Man Water wa Combinenga.
“Sijaelewa damond kupata tuzo 7 alafu produza wake kutoka na 0!!!!!” ni jibu la moja ya maswali kuhusiana na tuzo hizo aliyokutana nayo Master J Jana alipokuwa mgeni katika session ya ‘Kikaangoni Live’ kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV.

Shabiki mwingine aliuliza: “Pia man water ni mkali au unasemaje master J?”
Na hiki ndicho alichojibu Jay: “mkali lakini hakusahili kushinda mwaka huu”
Swali tofauti na muziki ambalo lilijirudia mara nyingi ni kuhusu uhusiano wake na mpenzi wake Shaa, shabiki mmoja aliuliza:
“Mnafunga ndoa lini ww na Shaa manake mnapendezana kweli? Au ni mchepuko tu wa lami?

Na jibu la Joachim aka Master J mabibi na mabwana lilikuwa “SOON”.

Related

BONGO FLAVA 7407614449311090431

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item