DISQUS SHORTNAME

RAY C AFUNGUKA

MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na...

MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi
Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’,
amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya
kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio ulioibuka
hivi karibuni wa Homa ya Dengue.
Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema
Chalamila ‘Ray C’, akiwa kwenye red carpet ya
Kilimanjaro Tanzania Music Awards.
Akifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya
kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala,

Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila
Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake
hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso
makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa
juzikati alipopata ugonjwa huo.
Alisema kwamba dakika chache tu baada ya
kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa
kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila
kuremba aliwasha gari lake na kukimbilia
Hospitali ya Mwananyamala.
Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele
alisema alipofika kwa kudra za muumba
alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu.
“Huwezi kuamini baada ya madaktari kunipima
na kugundua nina Ugonjwa wa Dengue,
walinishangaa sana hata namna nilipofika pale
na kwamba sikutumia dawa yoyote ya kutuliza
maumivu kwa sababu maumivu yake huwa ni
lazima utatafuta tu dawa ya kukufanya upoze
maumivu.
“Madaktari wengine wakatishika zaidi maana
walisema kama ukimeza vidonge vya ‘Diclopa’
unaweza kupoteza maisha mara moja.
“Katika magonjwa ya ajabu na yanayostahili
kutafutiwa kinga mara moja basi huu ni
ugonjwa wa kwanza ambao serikali inatakiwa
iwe macho sana maana haufai hata kidogo.
“Tena unatisha sana na wasipoangalia
utapoteza maisha ya Watanzania kibao kama
hawatautafutia kinga au kuwapa Watanzania
elimu ya kutosha.
“Mateso niliyoyapata kwa siku mbili nilizolazwa
Mwananyamala ni elimu tosha kabisa na
kwamba ningekuwa na uwezo wa kuzunguka au
kupata nafasi ya kuongea na wakuu wa nchi
basi mara moja ningewaomba wafanye jitihada
za haraka kuhakikisha wanapata chanjo kwa
ajili ya kuudhibiti mfumko wa gonjwa hilo.
“Dengue unaambukizwa na mbu tena wa
mchana na dawa yake ni panadol tu!” alimalizia
Ray C.

Related

BONGO FLAVA 4684390383052997317

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item