Diamond na Wizkid kutumbuiza jukwaa moja kwenye tuzo za MTVAfrica ‘MAMA’ Afrika Kusini wiki ijayo
Orodha ya wasanii watakaopanda jukwaani kutoa burudani katika tuzo za MTV Africa Music Awards (MAMA) inazidi kuongezeka, sasa MTV Base i...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/diamond-na-wizkid-kutumbuiza-jukwaa.html
Orodha ya wasanii watakaopanda jukwaani kutoa burudani katika tuzo za MTV Africa Music Awards
(MAMA) inazidi kuongezeka, sasa MTV Base imewataja ‘Number One’ hit maker Diamond
Platnumz, Wizkid na Phyno wa Nigeria pamoja na Yuri Da Cunha wa Angola kuwa miongoni mwa
wasanii watakaotumbuiza.
Diamond ambaye pia anawania tuzo mbili za ‘Best Collabo’ pamoja na ya ‘Best Male’ katika tuzo hizo, anaungana na wasanii wengine wa Afrika kama Davido, Flavour, Tiwa Savage,
Mafikizolo, Uhuru na Oskido ambao walikuwa wameshatajwa kutumbuiza. Wasanii wa kimataifa walioishatajwa kuperform siku hiyo ni pamoja na mwimbaji wa R&B Trey Songz, French Montana na Miguel. Host wa show hiyo atakuwa mchekeshaji na muigizaji wa filamu Marlon Wayans. Tuzo hizo zitafanyika wiki ijayo (June 7) katika ukumbi wa ICC huko Durban, Afrika Kusini na zitaoneshwa live kupitia MTV, MTV Base, BET International na vituo vingine washirika.


Kila la kheri watanzania tunakuombea!
ReplyDelete