DISQUS SHORTNAME

Masikini Mrembo huyu awezi Kubeba ujauzito!! ,sababu hii hapa

Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2001,Hapiness Millen Magese akiongea na waandishi wa habari kati...



Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2001,Hapiness Millen Magese akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam Mei 28,2014 kuhusu kuanzishwa kwa Kampeni ya kuhamasisha wanawake na vijana kupaza sauti zao wanaposumbuliwa na ugonjwa wa ‘Endometriosis’ baada ya yeye kuathirika na Ugonjwa huo kwa kipindi kirefu.
Amesema wanawake wengi na wasichana wamekuwa wakisumbuliwa lakini hawajui kama ni tatizo kubwa linalohitaji utafiti mapema kwa ajili ya kutafuta suluhisho. "Hili ni tatizo ambalo limenitesa tangu nikiwa na umiri wa miaka 13, na kuniathiri mpaka leo hii sina uwezo wa kupata mtoto kwa njia ya kawaida. Ila nina nafasi ya kuweza kupata mtoto kwa njia mbadala, mfano kwa njia ya kupandikizwa, au kupandikiza kupitia mwanamke mwingine kwa kutumia mayai yangu, na njia ya tatu ni kuasili,alisema Magese kwa ujasiri wa hali ya juu. Jumapili ya wiki hii  yeye na wataalamu watatoa mafunzo kwenye fukwe za Coco beach jijini Dar es salaam ambapo watu wataelimishwa athari na nini kifanyike ikiwa watagundulika kusumbuliwa na tatizo hilo.
Daktari bingwa wa masuala ya wanawake na uzazi ‘Endometriosis’ wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk. Belinda Balanda,  akielezea seli za mji wa uzazi zinazokuwa nje ya uzazi ambazo hushambulia eneo hilo na kumsababishia mwanamke maumivu makali wakati wa mzunguko wa hedhi. Waliohudhuria katika mkutano huo;



Related

HABARI YA MJINI 5073967115642899031

Post a Comment

  1. Jamani mimi naomba usaidizi mwezi niwa tatu sijaona damu yangu ya mwezi na sina mwana wala sija zaa waka sijaingiliwa je nifanye nini nawaombeni munisaidie

    ReplyDelete
  2. jamani itakua sangapi tuhudhuruie jaman maana wengi tunaumwa na hayo matumbo anaefaham pliz anijulishe

    ReplyDelete
  3. Nilikuwa na tatizo hilo kwa miaka mitano nikaelekezwa kwenda kwa Dr mmoja bingwa wamambo ya uzazi now im proud ninawatoto na waliokuwa na tatizo kama langu niliwaelekeza wakatibiwa pia mmoja wao ameshajifungua mtoto ana miezi 9 sasa.

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item