Masikini Mrembo huyu awezi Kubeba ujauzito!! ,sababu hii hapa
Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2001,Hapiness Millen Magese akiongea na waandishi wa habari kati...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/masikini-mrembo-huyu-awezi-kubeba.html
Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2001,Hapiness Millen Magese akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro,jijini Dar es Salaam Mei 28,2014 kuhusu kuanzishwa kwa Kampeni ya kuhamasisha wanawake na vijana kupaza sauti zao wanaposumbuliwa na ugonjwa wa ‘Endometriosis’ baada ya yeye kuathirika na Ugonjwa huo kwa kipindi kirefu.
Amesema wanawake wengi na wasichana wamekuwa wakisumbuliwa lakini hawajui kama ni tatizo kubwa linalohitaji utafiti mapema kwa ajili ya kutafuta suluhisho. "Hili ni tatizo ambalo limenitesa tangu nikiwa na umiri wa miaka 13, na kuniathiri mpaka leo hii sina uwezo wa kupata mtoto kwa njia ya kawaida. Ila nina nafasi ya kuweza kupata mtoto kwa njia mbadala, mfano kwa njia ya kupandikizwa, au kupandikiza kupitia mwanamke mwingine kwa kutumia mayai yangu, na njia ya tatu ni kuasili,alisema Magese kwa ujasiri wa hali ya juu. Jumapili ya wiki hii yeye na wataalamu watatoa mafunzo kwenye fukwe za Coco beach jijini Dar es salaam ambapo watu wataelimishwa athari na nini kifanyike ikiwa watagundulika kusumbuliwa na tatizo hilo.

.jpg)


.jpg)


Jamani mimi naomba usaidizi mwezi niwa tatu sijaona damu yangu ya mwezi na sina mwana wala sija zaa waka sijaingiliwa je nifanye nini nawaombeni munisaidie
ReplyDeleteNenda hospitali
Deletejamani itakua sangapi tuhudhuruie jaman maana wengi tunaumwa na hayo matumbo anaefaham pliz anijulishe
ReplyDeleteBG up dada
ReplyDeleteNilikuwa na tatizo hilo kwa miaka mitano nikaelekezwa kwenda kwa Dr mmoja bingwa wamambo ya uzazi now im proud ninawatoto na waliokuwa na tatizo kama langu niliwaelekeza wakatibiwa pia mmoja wao ameshajifungua mtoto ana miezi 9 sasa.
ReplyDelete