DISQUS SHORTNAME

VOTE ZA BET ZINAZOONESHA DIAMOND KUONGOZA NI ZA KITU CHA REDIO CHA V 101.9 CHA MAREKANI

Bila shaka umeshakutana na tweets au picha  kwenye Instagram inayoonesha upigaji kura wa  tuzo za BET ambapo kwenye kipengele cha Best In...


Bila shaka umeshakutana na tweets au picha  kwenye Instagram inayoonesha upigaji kura wa  tuzo za BET ambapo kwenye kipengele cha Best International Act: Africa, Diamond anaonekana kuongoza.
Well, ni good news kwa mashabiki wake lakini bad news ni kuwa kura hizo hazihusiki kabisa na kura zenyewe za BET kumpata mshindi. Kituo cha redio cha V101.9 cha Marekani  kimetengeneza utaratibu wake mwenyewe wa kuwapa nafasi wasikilizaji na wasomaji wake  kumpigia kura msanii wanayempenda na kura
hizo zitaishia kuwapa wao picha ya namna wasomaji wanapendekeza washindi wao. Kufanya  hivyo ni rahisi sana na hata sisi tukiamua kutengeneza ballots systems kama hizi ingewezekana. Utaratibu wa tuzo za BET upo tofauti kabisa na unaotumika kwenye tuzo zingine kama CHOAMVA  ama MTV MAMA ambapo baada ya majina kutangazwa, mashabiki huwapigia kura wasanii  wanaowapenda.  Kwenye tuzo za BET kuna jopo ama academy maalum yenye watu takriban 500 ambao ni wadau wa kiwanda cha muziki, habari na bloggers. BET huwataka watu hawa kupendekeza  majina kwenye kila kipengele kwa mfumo wa
kupiga kura ‘electronically’. Kura hizi husimamiwa na kundi liitwalo “Yangaroo” ambalo hufanya kazi kwenye tuzo  zingine pia. Kundi hili hupunguza majina na kubakiza wasanii watano kwenye kila kipengele na kuyatuma tena majina hayo (ambayo hutagazwa sasa rasmi kama majina ya mwaka husika) na kuyarudisha tena kwenye academy  hiyo itakayopiga kura za mwisho kupata mshindi.  Habari njema ni kuwa, Vanessa Mdee pia ni miongoni mwa member wa academy hiyo. Hivyo  bila wasiwasi atampigia Diamond. Haijulikani
kuna members wangapi Afrika Mashariki ambao kiuzalendo watatakiwa kumpigia kura Diamond.

Related

HABARI YA MJINI 1905716103167996884

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item