DISQUS SHORTNAME

AVUNJA NDOA YAKE KWA KUTAMANI MAISHA YA WEMA SEPETU

Kuiga ni kawaida kwa wengi.Wapo walioiga  mambo fulani na hatimaye wakafanikiwa, na  pia wapo walioiga vitu flani wakaharibikiwa.Huyu alii...

Kuiga ni kawaida kwa wengi.Wapo walioiga  mambo fulani na hatimaye wakafanikiwa, na  pia wapo walioiga vitu flani wakaharibikiwa.Huyu aliiga na akaharibu kila kitu...  Ni msanii wa siku nyingi katika fani.Alitamba zaidi akiwa Kaole, na hata mwanzoni mwa ujio wa filamu za Kanumba  alizidi tu kashaini.... Kiasili ni mweusi japo siku hizi kuna weupe fulani katika ngozi yake nyororo.Ana sura  nzuri yenye mvuto,umbo aslia la kibantu,meno yake meupe yamepambwa na mwanya mdogo na kufanya iwe fahari
kumuona akitabasamu...
Hana kashfa ya kuvaa nguo fupi sana ila  aliwahi kukumbwa na skendo kubwa
zaidi.Mkumbuke vizuri.Mrefu wa wastani,anajua kutembea,anaongea kwa mapozi huku akipenda kulamba papi ya  midomo yake. Umemjua???....Hapana, siyo huyo...!!  Huyu ni mpole kiasili na anapendwa sana
na mama yake.Katika maigizo ana uwezo wa kukufanya uamini unachoangalia ni kitu  halisi.Japo huwezi kumtaja, ila ndani ya wasanii kumi anapaswa kuwamo... Na ingawa mvuto wake umepungua kiasi,ila bado mrembo sana.Lakini wakati anaigiza Kaole alikuwa mrembo zaidi.Kwa uzuri  wake , alivuma na kila habari inayohusu mwanaume maarufu na mwenye pesa Habari ya kutakiwa na kila mwanaume , wenye rangi na vipato tofauti zilisikika kila kona.Baadhi alitoka nao na wengine haikuwa bahati yao....  Toka kitambo almanusura aolewe, ila ni miaka ya juzi juzi ndipo aliolewa.Uzuri wake si wa kutafuta, kila mwenye macho na
ngozi ya kuhisi atautambua.... Mbali na majanga yote aliyopitia katika  maisha yake,mengine yakibaki kumchafua na watu kudhani hawezi kuolewa na mwanaume  yeyote kabla ya ile bahati ya mtende
akaolewa; yeye aliamua kuachana na ndoa yake kwa kuona aishi katika umaarufu  wake.... Mara kadhaa alikuwa akiwaambia marafiki zake kuwa, mwenye hadhi na anayetakiwa  kuishi kama Wema Sepetu sio Wema bali ni yeye na wakongwe wengine waliosotea sanaa na kuipigania kama roho zao na kuilinda  kama mboni ya jicho lao.....  Akaona ndoa sio mahala pake,bila sababu za msngi akaamua kumwambia mumewe
watengane....Japo haikuwa rahisi ,lakini walitengana!!  Cha kufurahisha ni kwamba bado Wema anaishi kama Wema na bado yeye haishi kama Wema Sepetu na ndoa haipo tena...Umemjua ninayemzungumzia?
By: Blogu ya Wananchi

Related

STORY ZA KITAA 6551155105175448273

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item