DISQUS SHORTNAME

DIAMOND AANIKA SABABU 5 ZA KUMPENDA ZARI!

Mapenzi bhana! Baada ya kutoka kimalavu na kumwagana na mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kisha kuang...

Mapenzi bhana! Baada ya kutoka kimalavu na kumwagana na mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kisha kuangukia kwenye ‘utamu’ wa penzi la mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameamua kuanika siri tano za kilichomvutia kwa staa huyo gumzo Afrika Mashariki.
 Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady.
Akizungumza katika mahojiano maalum katika ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar hivi karibuni, bila kupepesa macho au kuuma maneno baada ya kuulizwa kinagaubaga juu ya ukaribu wake na Zari, Diamond au Dangote hakutaka kuficha, akaamua kuweka mambo yote hadharani.
MATANGAZO
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa na mwenye heshima, wakati mwingine natakiwa kuwa na akili ya kuwa na uhusiano na watu ambao watakuwa msaada kwangu pia.
“Siwezi kuwa karibu na mtu ambaye hataniongezea kitu chochote kile. Baada ya kujitangaza sana Tanzania, nikahamia Kenya ambapo nilikuwa karibu na mwanadada Avril. Ukaribu wangu kwake, ukanifanya Kenya kutambulika.
“Baada ya kukaa kwa muda, nikataka nitambulike na Uganda pia, unafikiri ningefanya nini? Nikaliteka soko lao kwa kuwa karibu na mrembo Zari.
“Kweli nimefanikiwa na hata siku ya shoo yake (Desemba 18, mwaka huu nchini Uganda), ilikuwa ni balaa kiasi kwamba sikuamini kilichokuwa kimetokea, watu walikuwa nyomi ile mbaya. Mbali na kuwa mwanamuziki mkubwa, bado nahitaji kujitangaza zaidi.”
 Zari na Diamondi wakibusiana kimahaba.
MSISIMKO
Sababu ya pili aliyoitaja ni kwamba Zari ambaye ni mama wa watoto watatu ana msisimko wa aina yake tofauti na ‘mashori’ wengine aliwaowahi kuanguka nao dhambini.
“Hakuna mwanaume anayependa kukaa na msichana asiyekuwa na msisimko wa kimapenzi. Hebu fikiria umekaa na mwanamke mwenye umbo kama la mwanaume, utapata msisimko gani hapo? Lakini mcheki mtoto alivyong’aa, anameremeta, mtoto yupo bomba, ukikaa karibu yake tu utagundua kwamba umekaa na msichana mwenye mvuto ambaye kila wakati atakufanya kuwa bize kumwangalia.”
BIASHARA
Sababu ya tatu aliyoitaja Diamond ni kwamba mwanadada huyo yupo vizuri kibiashara.
“Ninaangalia fedha, ili biashara zangu ziweze kupiga hatua sina budi kukaa karibu na mfanyabiashara mwenzangu (Zari) kwa ajili ya kushauriana biashara ziende vipi.
“Yeye (Zari) ni mkongwe katika biashara, kuwa karibu naye naamini nitajifunza mambo mengi sana.
Amekuwa muwazi kwangu na amenipa mianya mingi ya kufanya biashara, lakini je, nisingekuwa karibu naye, michongo hiyo ningeipata vipi?”

UZURI
Sababu ya nne ya kuwa na Zari, Diamond alidai kwamba mwanamama huyo ni mzuri kupita maelezo.
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa, watoto wazuri wananipenda kwa hiyo kama ningefanya uamuzi wa kuwa na mwanamke asiyekuwa mzuri, maneno yangeanza kusikikasikika na isingekuwa poa. Mbali na kuwa mfanyabiashara, kumtumia kama msaada wa kunitangaza, lakini Zari ni mzuri bwana. Ni mwanamke ambaye kwa kumwangalia tu, unaweza kusema kwamba haujawahi kukutana na mwanamke mzuri kama yeye.
ANAJITAMBUA
Sababu ya mwisho aliyoianika Diamond ni kwamba Zari yupo vizuri kichwani kwa maana ya kujitambua tofauti na wanawake wote aliowahi kutembea nao.

“Nimekuwa na wanawake tofautitofauti lakini kwa Zari, ni mwanamke mwenye hekima na anajitambua sana. Si mzungumzaji kivile na huwa anapenda kufanya vitendo kuliko maneno.
“Anajua ni kipi anatakiwa kufanya na akili yake ameielekezea kwenye fedha zaidi. Hapendi masihara na fedha, anapenda kujitoa na ni mchakarikaji sana. Nampenda mwanamke wa hivyo kwa kuamini kwamba atanifanya nijitume zaidi.”
AWACHAMBUA JOKATE, WEMA NA PENNY
Diamond alipoulizwa juu ya kasoro za warembo wakali Bongo aliowahi kutoka nao wakiwemo mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Wema na mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’, aliwachambua mmoja baada ya mwingine na kuhitimisha kuwa ni wazuri lakini hawamfikii Zari.

Related

MAGAZETI YA UDAKU 4767882804625707470

Post a Comment

  1. Cjui kma kweli maana magazeti nayoo yatubeba saana kwa ajili ya biashara,ili mladi wauze.ila kma kweli alifunguka hivi nina haya ya kusema,nasikitika nasibuc mkweli pia ameridhi tabia za baba yake kweli nimeamini dam ya mtu aiendi bure,baba yake enzi zake kule kariakoo alikua anawapanga bwana acha wa tandamti acha wa agrey hiyo ni mitaa nimeitaja kwa ufupi kwenye ma hall ya mziki alikua anagombaniwa ile mbaya ma bibic mchezo ,kwa mama zetu aliojitegesha kuzaa naye walikua kwenye wakati mgumu sana .maana alikua ashikiki akamatiki akua mwanaume wa kujali wala kushitushwa na jambo,akujali upendo wa mwanamke aliyemzalia ,yani alikua play boy.eat and run.

    ReplyDelete
  2. Nasikitika haya c maisha mazri aliyojichagulia,apingane na historia ya baba yake ,akuna mtu wa kukusaidia kwenye biashara zako ila ni ww mwenyewe ,kma unanona ufahamu wako umeishia hapo nenda shule ukasome masomo ya biashara na ubunifu ,utaongeza kitu,usimtegee mtu unaweza ukamtegemea akuongoze kweli akafanya hivyo lakini kwa manufahaa yake mwisho wa cku ukalia wanao kusapoti leo kesho watakucheka kwa kua uelewa wako mdogo tafahali kuwa makini,akuna anaetosheka na utajiri au mafaniko akuna dunian hapa,upande wa pili yy aliolewa na amezaa wtt3,mna gap kubwa sana yy na mumewe walifikia hapo unapomuona wameshindwana wenyewe wanasababu zao,lakin kaa ukijua huyo mwanamke ana majukumu ya kuakikisha anatafuta kwa ajili ya wanawe ili wawe na maisha mazuri baadae ata akifa kesho gafla ajua amewaacha katika nafasi nzuri,pia mtaraka wake kma mfanya biashara bac anafanya juu chini ili amuone anapanda kwenye biashara alizomuachia ,na hawezi kukufanyia ww nasibu mdogo wangu wasomi huwa wana akili ya ziada .ila muamuzi ni ww mwenyewe maana utajili wa kitoto hunasumbua akili sana,.

    ReplyDelete
  3. Jua nasibu mdogo wangu akuna mwanamke mzuri,utamaliza mabucha nyama ile ile ebu tafuta mke huoe upo kwenye kipindi cha hatari saana tutakupateza bado mdogo mnooo.kufilisika ni jambo baya sana ebu angalia mbele wenzetu wanamuziki wengine wamefiricka na walikua na ela.achana na mambo ya kina zari na urembo wao na utajili wao,wa maigizo utapotea ndg yetu tunakupenda saaana,.

    ReplyDelete
  4. Diamond, pongezi za dhati kwa jitihada zako zilizokuletea mafanikio makubwa katika Umri Mdogo ulionao...pongezi zaidi pia kwa kutuletea heshima kubwa kama Taifa! Umepeperusha vizuri bendera yetu Taifa- U made us proud. Mungu akubariki katika Kazi zako na siku zote.
    Baada ya hayo, ninaona ni stahili yangu kama mzazi kuongezea ushauri uliotolewa na mchangiaji wa 3 kwa kusema:
    Si Sawa kabisa wewe kujiingiza kwa Zari mzima mzima. Pengine amekuvutia kama mwanamke- Au Kaja Kwako kutafuta "kick" hasa baada ya kinachosemekana "kuachwa na. Mumewe" yote hayo ni juu yako kuyatafakari! Ninachosema ni kwamba:

    You don't fit anywhere in her equation. Ana watoto 3, leo hii sidhani atakuwa na interest tena ya kuzaa, tena mtoto wa nje ya ndoa. Kwa maana hiyo wewe kama kijana unayetamani sana mtoto itachukua kama mwaka mmoja Hivi (kama msipoachana within these 3 months or 100 hot, sweet loving days), kupata mwanamke mkaelewana hadi Ku-settle ndipo mpate mtoto. Ikifikia kipindi hicho huna hakika Kama utaendelea kuwa juu Kama sasa Au vipi? Kumbuka, kwa maisha ya sasa issue si kuzaa, ni kuzaa na nani? Mtoto atakuwa ktk malezi gani, shule gani,U mejiandaaje, na ukiishiwa wewe mama yake anaweza kuku-support wewe na mtoto/watoto? Ninakushauri tafuta mwanamke, awe wa ki tanzaniia, mwenye malezi, elimu ya kutosha ( na promising future) juu ya yote anayekupenda kiukweli, oa ndipo mzae. Usitafute wa kuzaa na wewe tu, hutapata mama mzuri wa watoto wako, na msichana yoyote hatakubali hiyo proposal kwa sababu haitakuwa na commitment. Je akizaa ukambwaga? Kuna wa kuoa wake waliozalishwa na wanaume wengine? Kila binti anatamani umheshimu kiasi cha kumuoa.

    Umesema vizuri: bibie yuko kibiashara zaidi. Hiyo ndiyo sababu kakufuata wewe, there must be a catch na anajua kwa sasa uko juu. Asingekusogelea Kama angekuwa vizuri kipesa. Kumbuka, hakuna mwanaume asiyependa mwanamke mzuri so ujue wote wanamtamani lakini hawajafika bei, Au wanamuogopa wanajua amezoea pesa nyingi.

    U- celebrity wa waimbaji wengi unaishia miaka 30, sana 35. Ningefurahi kukuona na mwanamke mzuri Kama Zari, lakini aliye-committed Kwako. Iwe hela ulizonazo sasa mnapeana ushauri ( as a couple) muwekeze vipi. Zari interest yake kwa sasa Lazima aielekeze ktk kujenga ngome yake, ili asionekane amelosti na Pia wanae waishi maisha bora na kupata elimu bora.

    Siamini Kama anakupenda. Sasa Hivi utatoa chochote uwe Naye, na Kama unavyojua anakotoka, rigwaride kwa. Sana. Anapenda ujana na nguvu zako. Pia Watu wa maeneo Yao wana dharau sana when it comes to a Tanzanian, jumlisha wewe hujasoma kihiivyo. Sishangai wanaandika hovyo Kwenye social networks baada ya wao kusikia uko nao. Hata ndugu yake wa kiume kamuuliza kuhusu wewe akasema 'he is just a friend' pekura mitandao utaona!

    Zari ni mzuri, na 'age is nothing but a number' when you are in love - sawa - lakini kwa kiafrika tunajali sana Umri wa mwanamke- ukitaka azae n.k. Hata interest tu mmeshapishana, mavazi, n.k. Kwa hayo yote assessment yangu itabaki- Kaa Naye Huku unatafuta wa kudumu. Kumbuka: Mwanaume hajisifii kwa umaarufu wa kubebwa na mwanamke- tena hayo maneno usiyarudie.

    NB: Mwanaume wa kweli hatoi Siri za wanawake zake (hata Kama amewaacha...) Huwezi kujua mipango ya Mwenyenzi Mungu.

    Ninaamini utayatafakari.

    Ninakutakia kheri na baraka tele za Mwenyenzi Mungu katika mwaka 2015 na siku zote.

    Ni Mimi, team Diamond!

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item