DISQUS SHORTNAME

Vurugu kubwa zatokea Kariakoo, Dar...

 Vurugu kubwa imetokea mda huu maeneo ya kariakoo Jijini Dar Es Salaam na kupelekea Jeshi la polisi kurusha Risasi hovyo ili ...




 Vurugu kubwa imetokea mda huu maeneo ya kariakoo Jijini Dar Es Salaam na kupelekea Jeshi la polisi kurusha Risasi hovyo ili kuwatawanya Wamachinga walioanzisha Fujo hizo huku barabara za kuingia na kutoka kariakoo zikiwa zimefungwa kutokana na Matairi ya Gari yaliyochomwa moto barabarani.

Kwa Mujibu wa Shudhuda wetu aliyoko Maeneo hayo ya Kaliakoo anasema Chanzo cha vurugu hizo zinatokana na Wafanyabiashara Wadogodogo Maarufu Wamachinga kudai mfanya Biashara mwenzao kuuliwa na Mgambo wa jiji.

Shuhuda huyo alizidi kusema Mfanya Biashara huyo aliuliwa na Mgambo kwa kupigwa kipigo kikali na kumpelekea mauti, Wafanyabiashara hao wanadai hali hiyo ni ishara ya kuchoshwa na Manyanyaso hayo wanayofanyiwa na Mgambo hao na kuanzisha hali hiyo ya Fujo ambayo wanadai ni njia ya kupeleka ujumbe kwa Serikali.

Related

ZILIZOTUFIKIA 4634279328601800559

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item