DISQUS SHORTNAME

JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA

Kwanza discipline au adabu ni kitu mhimu sana katika kitu chochote unachotaka kufanya,ue na adabu kwa Mungu wako na unwombe akusaidie kuf...


Kwanza discipline au adabu ni kitu mhimu sana katika kitu chochote unachotaka kufanya,ue na adabu kwa Mungu wako na unwombe akusaidie kufanya hicho unachotaka kufanya!!!
Sikiliza moyo wako:
Kitu unachofanya kwa amani na furaha siku zote kitafanikiwa hata kama 2 vita vipi,make sure moyo wako una amani na furaha hata huduma yako utaifanya kwa heshima na utatoa customer care nzuri,kama ni mipango ambayo bado haijawa halisi basi hata utekelezaji wake utakua na amani nao.
Andika mahali
Ukipata wazo ukahisi unaweza kulifanya au unaweza shirikiana na mwenzio kulifanya liandike mahali ikiwezekana bandika kabisa ili ukiingia ukitoka unalitizama na kulikumbuka,hata unaposali wakati unataka kulala unakumbuka kuliombea pia.
Usifanye kwa sababu flani anataka ufanye Kumbuka maono au mipango unayobeba ni wewe mwenyewe ndie unaweza kuyatoa vile unavyotaka,na sio kama flani anavyotaka,hata ukimwachia mtu afanye hatafanya kama unavyotaka ufanye!!! Tafuta suluhisho la tatizo Suluhisho la tatizo mahali ulipo ndio wazo namba 1 unalotakiwa kufanya,kutatua tatizo hilo ndio fursa yako kupiga hela.....mwenzio kafungua bucha wewe jirani hapo weka genge mtu akija kununua nyama anapitia viungo,akifungua duka la visu weka mahali pa kunolea visu lol,unajua Mungu alipoumba kila kitu hakukuumba na vitu kama kitanda au makochi alijua una akili sasa ulipotatua tatizo la kukaa ndipo ukaanza kuuza masofa,mfano ukiwa kazini mnaenda kula wapi ???! ni karibu ??? Hivi ukipika saani 5 ukaagiza ziletwe mda wa lunch ofcn ukauza 4 ukala 1 utakua hujasolve tatizo !?
Usisema ntafanya
 Fanya Kila kitu kina mda wa kuanza na mwisho wake,ukisikia una msukumo wa kufanya kitu mda huo fanya,huo upako juu yako ni wa Mungu ati na trust me atakusimamia na utaweza hata kama huna kitu watainuliwa watu hutajua wametoka wapi lakini utashangaa ukishafanya kua hivi ni mimi ndio nimefanya hiki !?? IT LOOKS IMPOSSIBLE UNTIL ITS DONE Ubunifu Kua mbunifu,usiige kwamba jirani kafungua duka la nguo anapata sana acha na mimi nfungue zitakudodea we hujui huyo alikuja na plan zipi kupata wateja,kua mbunifu njoo na kitu kipya ambacho hakitakua sawa na cha flani,na hili wengi limewaangusha na kupata hasara.
 Acha urafiki na biashara
Hata wewe ukichukua lipa,ndio ni biashara,marafiki zako wasigeuze kua kijiwe cha bureeeee....walipeeee !!! Hawataki wasepe ELIMU YAKO KIKWAZO Wengi walisoma ukiwaambia wakafungue mama ntilie hawataki kwa sababu wamesomea kitu kingine.....yaaakhhh...sikiza umesoma nursing ili ujue kua mteja akila sana akavimbewa mpe magnesium,ama ulisoma accounts ili ujue ukilipwa una credit ukitoa una debit,ulisoma uaskari ili jamaa asipolipa umshughulikie vizuri,Mungu sio zuzu wewe akupitishe koote huko halafu aku dump wewe hujielewi tu na ukiangalia hilo karatasi unaona you are a boss ....boss my feet !!! Hiyo ndio limit pekee inayokuzuia wewe kufanikiwa kama unabisha jaribu kufanya uone kama hujafanikiwa

Post a Comment

  1. Thanks Sana jipange,wtz wanahitaji Sana shule za namna hii.

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item