VIBWEKA VYA BIG BROTHER
Mghana amponda Idris, vituko vyatawala VITUKO vinazidi kutawala ndani ya mjengo wa Big Brother HotShots, Mghana Kacey, juzi alitoa kauli k...
Mghana amponda Idris, vituko vyatawala
VITUKO vinazidi kutawala ndani ya mjengo wa Big Brother HotShots, Mghana Kacey, juzi alitoa kauli kuwa Mtanzania Idris bado ni mdogo kiumri na hayupo makini katika mambo yake.
“Idris hayupo makini, anacheza mchezo huu kitoto. Nahisi mazingira ndiyo yanamfanya afanye yote hayo,” alisema mshiriki huyo wakati alipokuwa katika chumba cha mazungumzo na Biggie.
Luis ataka kujitoa Big Brother
Mshiriki kutoka Namibia, Luis juzi alionyesha nia ya kutaka kujitoa kwenye shindano ambapo alifikia hatua ya kukusanya kila kilicho chake na kuomba kuondoka. JJ na Idris walizungumza naye na kumpa ushauri wa kuendela kubaki mjengoni.
Idris ndiye ambaye alitumia muda mwingi kumbembeleza kutoondoka. Luis alionekana kuwa mpole na kutulia. Mpaka jana alikuwa hajaondoka.
Samanth na Mam Bea wapewa onyo
Washiriki wawili Samanth na Mam Bea, jana walipewa onyo na Biggie kwa kitendo cha kuzungumza siri ya wale waliowapigia kura za maoni ili waondolewe mjengoni.
Sheria za Big Brother ni kuwa chochote ambacho kinazungumzwa kwenye chumba maalum huwa ni siri. Biggie amewaonya wote kuwa atakayefichua siri ya mazungumzo katika chumba hicho ataondolewa mchezoni.
