DISQUS SHORTNAME

Chidi Benz akamatwa na dawa za kulevya airport

Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jiji...


Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini Mbeya kwenye show ya Instagram Party inayotarajiwa kufanyika kesho.

Shetta ambaye alikuwa naye pamoja katika safari hiyo ya kuelekea Mbaya, amethibitisha kukamatwa na kwa Chidi akiwa na vitu vinavyohisiwa ni madawa ya kulevya.
“Kweli tulipata matatizo na Chidi pale airport ila mimi nikaruhusiwa yeye nikamuacha, amekamatwa na mambo mambo fulani sema ongea na wahusika watakwambia zaidi,” alisema Shetta.
Akizungumza na Millard Ayo, kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Hamisi Selemani kamanda wa polisi katika uwanja wa ndege Dar es Salaam amesema Chidi Benz amekiri kuwa dawa hizo ni zake.
Amedai kuwa Chidi alikutwa na kete 14 za dawa za kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi iliyokuwa mifukoni mwake.
Chidi atapandishwa mahakamani hivi karibuni kwa kosa la kukutwa na dawa hizo.

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item