Sitti Mtemvu akanusha kuwa na mtoto, asema ana miaka 23, hatovuliwa taji
Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amevilaumu vyombo vya habari kwa kueneza habari za uongo kuhusiana umri na maisha yake binafsi. Mtemvu ...
Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amevilaumu
vyombo vya habari kwa kueneza habari za uongo
kuhusiana umri na maisha yake binafsi. Mtemvu
amesema hayo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu akiongea na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jumanne,
October 21
“Ukweli ni kwamba nina miaka 23 na cheti hicho
hapo kinajielezea, mkitaka mnaweza kwenda hizo
sehemu wanazotoa vyeti mkawauliza,” alisema Sitti.
Mtemvu alisema cheti chake cha zamani cha
kuzaliwa kilipotea akidai kuwa ni kutokana na
maisha yake ya kusafiri mara kwa mara.
Sitti Mtemvu na mama yake wakiondoka baada ya
kukutana na waandishi wa habari
“Kwahiyo ilibidi pale walipohitaji cheti nilete kingine,”
alijitetea.
“Sikutegemea hayo maswali leo kwahiyo sikuja
nimejiandaa kihivyo,” alijibu mrembo huyo baada ya
waandishi wa habari kumtaka awape ripoti yoyote
ya polisi kuhusiana na kupotea kwa cheti chake cha
mwanzo.
Cheti cha kuzaliwa alichonacho sasa kinaonesha
kuwa kilitolewa September 9 mwaka huu.
Hashim Lundega akionesha cheti cha kuzaliwa cha
Sitti Mtemvu
Sitti alitumia pia fursa hiyo kukanusha tetesi kuwa
ana mtoto. “Sina mtoto, na mkitaka tunaweza
kwenda hospitali sababu naona kama mmekuwa
mkiniandama kwa vitu ambavyo si vya kweli,”
alisema.
Akijibu swali la kuonekana kwa passport yake
inayoonesha kuwa alizaliwa mwaka 1989 na huku
kwenye cheti alichoonesha kikionesha amezaliwa
May 31, 1991, Sitti alisema:
Sitogusia hilo suala kwasababu mimi nilivyokuwa
nakuja kuomba ‘Umiss Tanzania’ niliombwa cheti
cha kuzaliwa sasa hivyo vitu vingine ni personal life,
kwahiyo sidhani hata nyie kama kuna mtu atakuja
anachukua passport yetu, ama driving licence ya
kweli au feki na kuiweka kwenye mtandao kama ni
kitu ambacho mngependelea.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Lino International
Agency Limited Hashim Lundenga alisema kuwa
nafasi ipo wazi kwa wale wenye mashaka na umri
na maisha ya Sitti kupeleka vielelezo halisi ambavyo
watavifanyia kazi.
Mkurugenzi wa Lino International Agency Limited
Hashim Lundenga akisisitiza jambo wakati
akizungumza na waandishi wa habari, kushoto ni
Miss Tanzania, Sitti Mtemvu
“Tukishapata proof tutazifanyia kazi vizuri sana na
mwenye haki atapata. Sisi hatuwezi kumvua taji,
vitahusika BASATA na wizara husika,” alisema
Lundenga.
Kuhusu Sitti kudanganya kuwa na umri wa miaka 18
kama watu walivyodai ndivyo alivyosema, Lundega
alidai kuwa hayo yamezushwa mtandaoni na kwenye
shindano hilo hakuna aliyesema hivyo.
“Unaamini kwamba Sitti ana miaka 18?” alihoji
Lundenga. “Sasa kama huamini yote yametoka
kwenye vyombo vya habari. Sisi tunaamini cheti cha
kuzaliwa, sasa kama kuna mtu ana doubt na cheti
cha kuzaliwa aende RITA akafanye uchunguzi wake.”
