DISQUS SHORTNAME

DIDA, EZDEN WAKUTANA COCO BEACH WAKAUSHIANA

WATANGAZAJI  wawili waliokuwa wanandoa kabla ya kutengana hivi karibuni, Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne, mwishoni mwa wiki walikaush...

WATANGAZAJI wawili waliokuwa wanandoa kabla ya kutengana hivi karibuni, Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne, mwishoni mwa wiki walikaushiana kama watu wasiofahamiana baada ya kukutana katika hafla iliyofanyika katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.

Khadija Shaibu ‘Dida’ akiwa ndani ya ofisi za Times FM.

Wawili hao walikutana wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo wa Namchukua wa Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambapo mwanaume alikuwa mshereheshaji huku mke akiwa miongoni mwa wageni waalikwa.

Mtangazaji wa TV1, Ezden Jumanne.

Hata hivyo, Dida alionekana kuwa na mbwembwe zaidi huku akipiga ulabu na kuonekana kukolea kiasi cha kujiachia na kukata mauno mbele ya halaiki ya watu pasipo kujali uwepo wa mumewe huyo wa zamani, ambaye alikuwa mpole na aliondoka eneo hilo mara tu baada ya kumalizika kwa shughuli iliyompeleka.

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item