Wolper akanusha kuyumba kwasoko la filamu baada ya Kanumba kufariki....Je wewe mdau unasemaje kuhusu hili?
Msanii wa filamu, Jacqueline wolper amekanusha mtazamo wa baadhi ya watu wanaodai kuwa baada ya kufariki Steven Kanumba, filamu hazifany...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/wolper-akanusha-kuyumba-kwa-soko-la.html
Msanii wa filamu, Jacqueline wolper amekanusha
mtazamo wa baadhi ya watu wanaodai kuwa
baada ya kufariki Steven Kanumba, filamu
hazifanyi vizuri.
Jacqueline wolper
Akizungumza na Sporah Show, Wolper alisema
watu wanaosema filamu hazifanyi vizuri baada ya
Kanumba kufariki hawafuatilii vizuri filamu
zilizopo sokoni.
“Ngoja nisawazishe hapo, kila mtu ana mashabiki
wake, ana msanii wake. Kuna mtu anaweza
akawa anampenda Kanumba tu,hampendi mtu
mwingine yeyote. Kwahiyo alikuwa anachukua
movie za Kanumba tu na kuna mtu mwingine
anaweza akawa anampenda Wolper tu unajuee!
Unajua kuna mashabiki wa hivyo ambao wale
mashabiki wanaingia hata front kupigana
ukimsema Wolper,ukimsema nani? sijui nani? You
know! Kwahiyo mimi ninaweza nikasema huyo ni
shabiki yake sana Kanumba. Kwahiyo anaona
Kanumba amekufa basi ndio kila kitu kimekufa.
Mimi kama juzi hapa nimefululiza kufanya kama
movie tatu hivi na Ray,wale ambao wanasema
zimeshuka labda hawajapitia madukani kuangilia
lakini movie zipo nyingi,” alisema.
Pia Wolper amesema anachukizwa sana na team
za kwenye mtandao wa Instagram zinazotukana
watu huku akizipachika jina la team ushuzi.
“Mimi ni family watu wangu wanajiita
family,siwajui,wengine wapo Kenya,wengine wapo
wapi? Kama kuna huyo Wolper family yule
aliniomba kabisa. Mimi sipendi team na kuna siku
nilirekodi video nikasema not team chochote.
Mimi nipo mimi kama mimi nasimama mimi kama
mimi. I hate team kwasababu hao team ushuzi
hawana kazi wanakaa wanatukana watu.
Unamtukana Wolper, you know my name ,you
don’t know my life! Why unakunja nne kwenye
kochi lako unakuwa unamtukana Wolper, mimi
nawaita tu ma team ushuzi, mimi sijui
wanalipwa, mtu anakaa anaandika Wolper anakaa
chumba kimoja na ana gari moja likiharibika ndio
basi tena.”

Ukweli upo wazi mambo yote enzi za kanumba
ReplyDeleteNi ukweli usio fichika sasa hivi mnacheza michezo ya kuigiza na sio movies angalau kidogo kanumba alikua anajaribu.
ReplyDeleteMi nakerwa na wasanii wa bongo baadhi yao hawajui kutamka herufi za maneno ya kiswahili vizuri siku moja nilikua na rafiki zangu wakenya tunaangalia mchezo wa kiswahili walinibeza wanasema kiswahili kimezaliwa tz lakini hatujui kukitumia vizuri kiswahili Kwa mf: mtu anakwambia niko balabalani au nimelamba Hii si sahihi tujaribu kufanya vizuri kwenye movies zetu.
ReplyDelete