DISQUS SHORTNAME

William Mtitu Ajenga Nyumba YaMilion 178.

Filamu zinalipa ! producer na muigizaji wa filamu  wa siku nyingi nchini William Mtitu amejenga  nyumba mpya ya kisasa maeneo ya Kigogo j...


Filamu zinalipa ! producer na muigizaji wa filamu  wa siku nyingi nchini William Mtitu amejenga  nyumba mpya ya kisasa maeneo ya Kigogo jijini Dar es salaam. Nyumba hiyo ambayo bado haijakamilika mpaka sasa tayari imegharimu kiasi cha shilingi milioni 178 za Tanzania.
Chanzo kimoja makini kikizungumza na GPL kilisema kuwa Mtitu alinunua kiwanja cha  nyumba hiyo kwa Milioni 45, milioni 38 kununua
samani za ndani na milioni 85 katika ujenzi. Mtitu mwenyewe ambaye ana filamu nyingi  sokoni zinazotamba alipotafutwa kuongelea suala hilo alisema kuwa hana la kusema kwa kuwa kila kitu kinajionyesha.  Mwaka jana Mtitu aliamua kuanza kusambaza filamu zake mwenyewe baada ya muda mrefu filamu zake kusambazwa na msambazaji mmoja ila Mtitu kudai alijitoa katika kampuni hiyo kuepuka unyonyaji wa wasanii uliokithiri ikiwemo kununua haki zote za msanii anapotengeza filamu. Hii inaweza kuwa moja ya sehemu ya kujifunza kwa baadhi ya wasanii ambao licha ya kuwa  tayari na uwezo wa kusambaza kazi zao
wenyewe lakini bado wamebweteka na kuishia kulalamika kila siku kuwa wananyonywa. Angalia  picha za mjengo wa Mtitu ambao bado kukamilika.......

Related

BONGO MOVIE 2594957155684382752

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item