DISQUS SHORTNAME

UCHAWI ’ WATAJWA PENZI LARAY , CHUCHU

‘UCHAWI ’ umetajwa kwenye mapenzi ya staa  wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘ Ray ’ na  ubavu wake wa sasa , Chuchu Hans.Staa wa filamu Bo...


‘UCHAWI ’ umetajwa kwenye mapenzi ya staa  wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘ Ray ’ na  ubavu wake wa sasa , Chuchu Hans.Staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray ’ akiwa na mpenzi wake Chuchu Hans .
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mapenzi ya Ray kwa Chuchu ni makubwa sana kiasi kwamba hayawezi kuwa ya hivihivi tu kwani  msichana huyo ni mtoto wa Kitanga anayejua  jinsi ya kumshika mwanaume kama Ray .
“Unajua siku moja niliongea na mtu, sitaki  kumtaja jina.
Akasema anaamini mambo ya ‘ kiswahili ’ yapo katika mapenzi ya wawili  hao, si rahisi Ray akawamwaga akina Johari ( na Mainda ) na kubaki na Chuchu tu . “Yule Chuchu ni mtoto wa Kitanga , watoto wa Kitanga ni waja leo waondoka leo , wanajua mambo mengi sana kuhusu mapenzi,wapo akina Mwakipesile walikwenda Tanga kufuata biashara ya nazi hawakurudi Mbeya, ”kilisema chanzo hicho. “Kama mtakumbuka waandishi , siku moja kwenye magazeti yenu mliandika kwamba Ray amesema hana mpango wa kumuoa Chuchu, lakini juzi tu kamvisha pete ya
uchumba kwa hiyo sasa uchumba wao ni rasmi . “Halafu kama mtakumbuka tena katika habari ileile, mlimuuliza Chuchu kuhusu madai ya Ray kwamba hana mpango wa kumuoa , alijibu Ray hana ubavu huo , yaani wa kutomuoa. Sasa niambieni , mtu ambaye hana mpango wa kumuoa demu , kwa nini amvishe
pete ya uchumba ?” kilihoji chanzo.Kikaendelea : “Hata kwenye tasnia ya filamu ,wengi wanasema mapenzi ya Ray na Chuchu yana ‘ kamzizi’ si bure maana jamaa ameoza kuliko inavyotakiwa . ” Baada ya taarifa hizo , juzi Amani lilimsaka Ray na kubahatika kukutana naye kwenye Gym moja iliyopo Kinondoni jijini Dar ambapo alipoulizwa kuhusu madai hayo hakupenda kutoa ushirikiano wowote ule , akasingizia anawahi hospitali ana Homa ya Dengu. Chuchu alipatakana nje ya Meeda Club Jumamosi iliyopita ambapo alipoulizwa alisema : “Kwanza nyiye mbona mnapenda sana kuwafungukia watu bila wao kujifungukia
wenyewe? Acheni watu wafunguke wenyewe bwana.” Hata hivyo , ni kweli Chuchu Hans ana pete
ya uchumba kwenye kidole kinachohusika .

Related

BONGO MOVIE 3624900080681032350

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item