DISQUS SHORTNAME

Tazama jinsi Jay Z akipigwa nashemeji yake (Solange) wakiwakwenye lift na Beyonce pembeni

Ni video kamili ikionyesha kilichotokea kwenye lifti ambapo rapper Jay Z anaonekana akipigwa na shemeji yake ambae ni Solange kwa muda u...


Ni video kamili ikionyesha kilichotokea kwenye lifti ambapo rapper Jay Z anaonekana akipigwa
na shemeji yake ambae ni Solange kwa muda usiopungua dakika 2 kwa kutumia pochi na  mateke na baada ya hapo wakatoka nje ya lift. Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, haya yalitokea wiki iliyopita kwenye After Party ya Met Gala ndani ya Standard Hotel, NYC na ndani ya video inaonesha Jay Z, Beyonce na Solange wakiingia katika Lifti halafu Solange anaanza kumuwakia Jay z kabla ya kuanza kumvamia wakati huo Beyonce akiwa pembeni tu ametulia na wala haingilii.

Bodyguard aliekuemo katika lifti hiyo alianza
kumzuia Solange lakini alifanikiwa kuponyoka  kama mara tatu hivi na kuendelea kumpiga Jay
Z pia kuna muda Solange alirusha teke na Jay Z akazuia lakini hakurudisha kwa aina yeyote
ile, sio kwamba alishindwa kumpiga ili alifanya maamuzi ya kuwa mstaarabu tu.  Moja kati ya picha za Jay Z na Solange Beyonce alikua amesimama tu bila kufanya chochote kile ambapo mpaka sasa bado haijulikani sababu ya ugomvi huo ambapo walipofika floor ya 12 bodyguard alibonyeza  kitufe cha dharura (emergency button) ili kuficha yanayotokea na kisha baadae wote watatu walitoka hotelini hapo huku Solange akionekana kukasirika, Beyonce akijaribu kuonyesha smile kwa mbali huku Jay Z akionekana kukasirika kabisa na hata kuwatolea nje mashabiki waliokua wanataka kumbukumbu. Beyonce na Solange waliingia kwenye gari moja na Jay Z alipelekwa kwenye gari jingine  na bodyguard ambapo mpaka sasa chanzo
kamili cha ugomvi huo bado hakijajulikana. Hizi hapa chini ndio video mbili za ilivyotokea
ambapo video ya kwanza inawaonyesha wakiwa kwenye lift na video ya pili wakiwa
wanatoka nje ya hoteli baada ya ugomvi kutokea.

Related

KWINGINEKO DUNIANI 1755073602900427463

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item