DISQUS SHORTNAME

KINARA WA MTANDAO WA WIZI KATIKA MABENKI JIJINI DAR ES SALAAM HUYU HAPA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum D ’ Salaam  limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu  ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi katika  mabenki ambay...


Jeshi la Polisi Kanda Maalum D ’ Salaam  limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu  ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi katika  mabenki ambaye anajulikana kwa jina la RONALD S /O MOLLEL umri miaka 37 , mfanyabishara na mkazi wa Kimara Bonyokwa Jijini D ’ salaam. Mtuhumiwa huyu amekimbilia mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi la  Benki ya Barclays Kinondoni lililotokea tarehe
15/4/2014 ambapo majambazi walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha  T. Shs. 390, 220 , 000/= , USD 55, 000 /= na EURO 2150 /=.
Aidha sasa imefahamika  kwamba mtuhumiwa huyu ni mume wa
mtuhumiwa wa kwanza katika tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D /O  KASILILIKA @ ALUNE D /O MOLLEL , miaka 28, Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la Barclays Kinondoni. Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila hali  kwa vile yeye ndiye alikuwa kinara wa  kupanga tukio hilo la Barclays na mara baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha  fedha hizo zilizoibiwa . Jeshi la Polisi limelazimika kutoa picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzi shirikishi ili mtuhumiwa huyu akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi ikiwa ni lengo la polisi kupambana na uhalifu katika dhamira ya kuzuia uhalifu , kulinda maisha na mali za wananchi . Zawadi nono ya fedha taslim itatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyu. Pamoja na maelezo hayo mtuhumiwa mwenyewe sasa anapewa fulsa
ya kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kabla ya kukamatwa kwa njia nyingine .

Related

HABARI YA MJINI 2253734909192506151

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item