DISQUS SHORTNAME

NORA AELEZA ALIVYOTESWANA PICHA ZA UTUPU

Tunaendelea kupata mtiririko wa mahojiano  ya mwingizaji Nuru Nasoro ‘ Nora’ tuliyoanza  wiki iliyopita , karibu : Mwigizaji mkongwe wa t...


Tunaendelea kupata mtiririko wa mahojiano  ya mwingizaji Nuru Nasoro ‘ Nora’ tuliyoanza  wiki iliyopita , karibu : Mwigizaji mkongwe wa tasnia ya filamu za  kibongo Nuru Nasoro ‘Nora ’
Gladness: Unawaambia nini wenzako wenye tabia hizo chafu za kutembea na watu ovyo ?
Nora: Mimi nawaasa waachane na tabia hiyo kwani magonjwa ni mengi ukizingatia kuwa wanaume wenyewe wanawatumia tu kama vyombo vya starehe .

Gladness: Ni kitu gani ambacho kimewahi kukuumiza sana katika maisha yako ?
Nora: Ukweli picha za utupu ziliniumiza sana kwani zilikuwa ni mbinu za wasanii wenzangu kutaka kunishusha kisanaa ambapo walinipiga nikiwa nimelala sijielewi .
Gladness: Huwa unaenda msikitini?
Nora: Ndiyo, mara mojamoja kwani mara nyingi huwa naswali nyumbani kwa siku  mara tano.
Gladness: Kwa nini msikitini mara mojamoja?
Nora: Dini yetu inaruhusu mwanamke kuswali  nyumbani kwani ndiyo anapata thawabu  zaidi .
Gladness: Uliwahi kuwa na bifu na Vincent Kigos ‘ Ray ’ na Blandina Chagula ‘ Johari’ , je  kwa sasa mkoje?
Nora: Mimi nilishawatangazia msamaha kwa yote mabaya waliyonitendea , Johari huwa  tunaongea lakini Ray sijawahi kuongea naye .
Gladness: Zamani uliwahi kuwa kichaa na kupotea kabisa kwenye fani , je  unayazungumziaje maisha hayo ya nyuma ?
Nora: Huwa sitaka kuyakumbuka kwa sababu  yananisikitisha sana , nilipoteza muda mwingi  sana na kurudishwa nyuma kimaendeleo .
Gladness: Ni mafanikio gani uliyoyapata  kwenye sanaa mpaka sasa ?
Nora: Sijapata mafanikio yoyote zaidi ya  kujulikana kwa sababu sanaa ya Tanzania  bado iko nyuma , hailipi kihivyo kama wa tu wanavyofikiria.
Gladness: Nini sababu za kuachana na mume  wako wa kwanza, marehemu Ng ’ wizukulu  Jilala?
Nora: Huwa sipendi kuzungumzia sana hilo ila kilichosababisha mimi kuachana na mume  wangu wa kwanza ni kwamba alikuwa akinitesa sana yaani nilikuwa nashushiwa  kipigo kila kukicha .
Gladness: Je , ulipewa talaka au uliamua  kuondoka tu mwenyewe ?
Nora: Ukweli baada ya kuona mateso  yamenizidi niliomba talaka mwenyewe lakini  aliitoa kwa nguvu baada ya wazazi wangu kuingilia kati .
Gladness: Ulifanikiwa kuzaa naye watoto  wangapi?
Nora: Nilifanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja  tu ambaye ndiye niliye naye mpaka sasa .
Gladness: Tuachane na mume wa kwanza tuje kwa huyu wa pili ( Luqman) , nataka kujua  je , yeye hukufanikiwa kuzaa naye ?
Nora: Hatukufanikiwa kuzaa , nami sikuwa  tayari kuzaa naye kwa sababu kuna vitu  ambavyo vilikuwa havijatimia .
Gladness: Baada ya kuachana na Luqman uliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na  msanii mwenzako Geofrey na mliahidi kwamba mtaoana lakini mkaachana , nini sababu?
Nora: Mimi sikuwahi kuwa na uhusiano na Geofrey yule alikuwa ni meneja wangu na tulikuwa tukishirikiana katika kazi .
Gladness: Je kwa sasa una mchumba au mpenzi?
Nora: Sina mpenzi wala mchumba.
 Gladness: Wewe ni mwanamke uliyekamilika unawezaje kuzuia tamaa za mwili wakati hauna mpenzi?
Nora: Huwa ninafanya mazoezi sana hivyo naweza kuzizuia tamaa hizo za mwili .
Gladness: Je una mpango wa kuzaa tena ?
Nora: Ndio, nikishaolewa nitazaa lakini siwezi kuzaa nje ya ndoa .
Gladness: Je unahitaji mwanaume wa aina gani?
Nora: Namuhitaji mwanaume atakayenipenda mimi Nuru na siyo Nora , mwenye mapenzi ya kweli , atakayeniweka mimi mbele kwenye kila jambo , anayejishughulisha kimaisha, mtanashati na anayemuogopa Mungu .
Gladness: Turudi nyuma kidogo kwenye kipindi ambacho uliugua sana na kuwa kichaa , je ni wasanii gani waliokuwa bega kwa bega na wewe ?
Nora: Hakuna hata mmoja aliyekuja hata kuniona zaidi walikuwa wakinikandamiza . Mwisho !

Related

BONGO MOVIE 5312338102704756734

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item