DISQUS SHORTNAME

AUDIO: Ni Wanachuo wa UDOM sasa,walichosema kuhusu kulala/kujiuza kwa baadhi ya Wabunge

Ripota wa nguvu Simon Simalenga akiwa  104.4 Dodoma amekutana na Wanachuo  kwenye chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo kwenye bunge la baj...


Ripota wa nguvu Simon Simalenga akiwa  104.4 Dodoma amekutana na Wanachuo  kwenye chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo kwenye bunge la bajeti linaloendelea May 19 2014 Wabunge walipitisha bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ambayo ni Bilioni 799.2 Ndani ya saa 24 toka kupitishwa kwa bajeti hiyo taarifa zinapatikana kwamba kuna  uwezekano wa kutokea maandamano ya  Wanachuo wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kuelekea bungeni kama hawatopata fedha zao  za kujikimu ambazo wamecheleweshewa kwenye collage yao ya Humanities. Wanasema ‘hatujazungumza hivi sababu tumepanic, kikawaida chuoni tunatakiwa kusaini boom kila baada ya siku 56 ambazo  ziliisha 26 April 2014 na mpaka hatujapata taarifa yoyote toka wakati huo kwamba kuna  shida gani imetokea’ 
Mwajuma Ally ambae ni Mwanachuo wa UDOM pia amesema ‘niko mwaka wa pili, tunashindwa kuelewa kwa nini hili tatizo  limetokea mpaka sasa hivi inaonekana sisi tunadharaulika manake hii ni mara ya pili  inatokea humanities lakini vyuo vingine wamepewa mikopo’ Wengine wanasema ‘Wanaume wenyewe sisi  wapiganaji mpaka sasa tunaumia… watoto wa kike je?’ Mwananchuo mwingine aitwae Upendo amesema ‘hii kashfa ya watoto wa kike kujiuza kwa Wabunge ni ya kweli kwa sababu boom  likichelewa ni bora nikakae maeneo ya bungeni kwa sababu nikimuelezea Mbunge nina shida  nitalala nae atanipa hela’  ‘Ndio maana Wasichana wengi tunapenda kujiuza, sio kwamba tunapenda kufanya makusudi ila ni kwa sababu tunacheleweshewa
hela na maeneo ya bungeni ndio tunapendelea kwenda kwa sababu tunajua kule ndio kuna mpunga mwingi kuliko sehemu nyingine’ Kwenye ofisi za utawala za chuo hicho Profesa  Mbunda akatoa ufafanuzi kwa kusema ‘kifupi ni kwamba management ya chuo kikuu  inafatilia hilo swala, afisa wake wa juu kabisa
wa mambo ya pesa yuko Dar es salaam na ameahidiwa katika siku tatu hili swala litakua  limetatuliwa kwa hiyo tunaomba Wanachuo wetu wavumilie kwa siku tatu’

Related

STORY ZA KITAA 3451033921199877806

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item