DISQUS SHORTNAME

Mwanamke aliehukumiwa kifokwa kubadili dini na kuolewa namume Mkristo

Mahakama nchini Sudan imemuhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanaume mkristo. Daktari Mariam Yahya ...


Mahakama nchini Sudan imemuhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanaume mkristo. Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag ambae baba yake ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume mkristo kitu ambacho
dini ya kiisilamu imeharamisha kwa Wanawake.
BBC wamesema Mariam mwenye umri wa miaka 28 pia ni mjamzito na  taadhabiwa kwa kuchapwa mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa. Unaambiwa Mariam alilelewa na mama yake mzazi ambae ni Mkristo lakini maafisa wa Sudan wanasema yeye bado ni Muislamu kwa sababu ndio dini ya baba. Alipewa siku tatu baada ya kuhukumiwa aweze kurejea katika dini ya kiisilamu lakini akakataa na ndio maana adhabu ikabaki palepale kwa kuwa Wanawake Waislamu hawaruhusiwi kuolewa na Wanaume Wakristo ingawa Wanaume Waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa
wanawake wakristo. Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International
linasema kuwa Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi kwa sababu baba yake hakuwepo naye maishani mwake. Kesi ya Ibrahim ni ya kwanza ya aina yake kusikika nchini Sudan kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters na Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamelaani uamuzi huo wa Mahakama na kuitaka serikali ya Sudan kuheshimu haki na uhuru wa watu kuabudu. Maafisa wa balozi za mataifa ya magharibi pia wamekemea vikali kesi hiyo na kuelezea asiwasi wao na kuwataka maafisa wa sheria nchini
humo kuangalia kesi hiyo upya na kuhakikisha kuwa Mariam anatendewa haki. Waziri wa mawasiliano amesema kuwa sio Sudan peke yake ambako sheria za kiisilamu zinafuatwa na ambako sio
sawa kwa mtu kubadili dini yake, hali hiyo pia ipo nchini Saudi Arabia na katika nchi nyngine zinazofata sheria za kiisilamu. Serikali ya Rais Omar al-Bashir inakabiliwa na changamoto nyingi za
kiuchumi na kisiasa hasa baada ya kujitenga na Sudan Kusini ambako mafuta yake yalikuwa yanatoka mwaka 2011.

Related

KWINGINEKO DUNIANI 9205031280576867689

Post a Comment

  1. wanaume wasenge sana wanatumia dini kuwakandamiza wanawake. wacha wazungu watuite manyani maana kwa style hii hatuna tofauti.

    ReplyDelete
  2. uhuru wa kuabudu jmn, khaaaaaa nchi nyngne bora ckuzaliwa huko

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item