DISQUS SHORTNAME

Mvua ya Samaki Sri Lanka

Samaki waliotoka mtoni kutokana na upepo mkali  Wakaazi wa kijiji kimoja Magharibi mwa Sri  Lanka wamesema kuwa wameshangazwa na pia kufu...


Samaki waliotoka mtoni kutokana na upepo mkali  Wakaazi wa kijiji kimoja Magharibi mwa Sri  Lanka wamesema kuwa wameshangazwa na pia kufurahishwa na tukio la 'kunyeshewa' na mvua  ya Samaki wadogo. Samaki hawa ambao walikuwa katika hali nzuri  ya kuweza kulika wanaaminika kuwa walibebwa
kutoka kwa mto kwa upepo mkali. Wanakijiji hao wa wilaya ya Chilaw walisema  kuwa walisikia kitu kizito kikianguka na wakapata samaki wengi wenye uzani wa kilo hamsini .
  Hili si tukio la kwanza la aina hii kuwahi kutokea Sri Lanka- mwaka wa 2012, kulitokea kisa cha  mvua ya viumbe vya baharini vijulikanavyo kama 'Kamba' ambavyo huliwa  Wanasayansi wamesema kuwa mvua ya Samaki  hutokea wakati ambapo upepo mkali unazinga juu ya maji ya kina kifupi na hivyo kusababisha  mzunguko wa maji unaovuta karibu kila kitu kilicho ndani ya maji ikiwa ni pamoja na samaki  na hata Vyura.  Wakazi wanasema sio mara ya kwanza kwa mvua ya Samaki kuwanyeshea Viumbe hawa wa majini wanaweza  wakasafirishwa kwa masafa marefu kwa kushikiliwa na mawingu hata baada ya ule mzunguko wa maji kuisha.  Wanakijiji wanasema kuwa mvua hiyo ya Samaki ilinyesha Jumatatu huku viumbe wale wakianguka kwenye mashamba, barabara na paa za kijiji hicho.  Baadhi ya samaki hao wenye urefu wa kati ya  sentimita tano na nane, walikuwa bado wako hai na walitiwa kwenye ndoo za maji na wanakijiji  waliowatumia kama kitoweo badaye. Hii ni mara ya tatu kwa tukio kama hili kufanyika  Sri Lanka, ingawa katika eneo tofauti.  Kando na ile mvua ya ‘Prawn’ya mwaka wa 2012 kusini mwa Sri Lanka, mvua ya kimondo (meteors) nyekundu na manjano ilinyesha mwaka huo huo,tukio ambalo bado linachunguzwa na  wanasayansi wa Marekani na Uingereza. Samaki wamadhamana kuu Sri Lanka.
Source: BBC

Related

KWINGINEKO DUNIANI 4884713383648405308

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item