DISQUS SHORTNAME

MUME WA JACK PATRICKAMNASA SALHA ISRAEL....NI MISS TANZANI 2011

SIRI imefichuka! Mume ( bado talaka ) wa mwanamitindo maarufu Bongo ambaye kwa sasa yuko korokoroni Macau nchini China kwa msala wa kukam...


SIRI imefichuka! Mume ( bado talaka ) wa mwanamitindo maarufu Bongo ambaye kwa sasa yuko korokoroni Macau nchini China kwa msala wa kukamatwa na unga , Jacqueline Fitzpatrick Cliff, Abdulatif Fundikira ‘ Tifu ’ anadaiwa kumnasa kimalavu Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Tifu ,
wawili hao hivi sasa wako kwenye ‘ mahaba niue ’ na wote wawili wako tayari kufunga ndoa kwani wazazi wa pande zote wamebariki ndoa hiyo . “Salha sasa hivi humwambii kitu kwa Tifu na kila mmoja yuko tayari kwa ajili ya kufunga ndoa na mwenzake. Lakini sisi kama marafiki wa karibu tunaona ni jambo la heri, ” kilisema chanzo hicho Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa huko nyuma Tifu alikuwa hana imani kabisa na wanawake tena baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito na aliyekuwa mke wake, Jack Patric, kiasi ambacho alisema hawezi kuoa tena . Rafiki huyo alisema kuwa baada ya Tifu kukutana na Salha aliona ndiye anaweza kuwa mke bora ( wife material ) na kuamini kuwa hawezi kumtenda kama alivyofanyiwa
huko nyuma . Baada ya kupata taarifa hizo , gazeti hili lilimtafuta Tiff ili kupata ukweli wa madai
hayo ambapo bila kukanusha alisema kuwa ni mapema kulizungumzia hilo kama yatakuwa
tayari ataweka wazi. “Kwa kweli hilo jambo ni mapema mno kulizungumza kwa hivi sasa lakini mambo
yakikuwa tayari nitaweka wazi kila kitu, ” alisema Tifu . Mwanamitindo Jack Patrick. Kwa upande wake Salha Israel alipopatikana kwa njia ya simu na kuelezwa kuwa Ijumaa Wikienda lina hadi picha zao za kimahaba alifunguka: “Ni kweli namfahamu , ni mtu wa karibu lakini ni sawa na kaka yangu pia . Hayo mengine labda mumuulize yeye.”

Related

HABARI YA MJINI 2779191627650159542

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item