DISQUS SHORTNAME

MUME WA FLORA MBASHA ASAKWA KWA UBAKAJI

JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha  ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa ny...


JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es
Salaam linamsaka kwa udi na uvumba
Emmanuel Mbasha  ambaye ni
mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za
Injili nchini , Flora Mbasha kwa madai ya
kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17
( jina tunalo) ambaye ni yatima .
Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo
kupitia vyanzo vyetu makini zinadai kwamba
mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo
Jumatatu iliyopita muda wa mchana na
kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na . TBT /
RB/3191 /2014 na ya Jalada la Uchunguzi
Na. TBT /IR/1865 /2014 akidai kufanyiwa
unyama huo kwa siku mbili ( Ijumaa na
Jumapili) wiki iliyopita nyumbani kwa
Mbasha , Tabata -Kimanga , Dar .
Ilidaiwa kuwa , Ijumaa iliyopita mlalamikiwa
alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na
Jumapili ilidaiwa alitekeleza ukatili wake huo
ndani ya gari lake hali ambayo ilimfanya
mlalamikaji kutoa taarifa Kituo cha Polisi,
Tabara -Aroma jijini Dar .
Iliendelea kudaiwa kuwa , kufuatia maumivu
makali aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi
aende Hospitali ya Amana na kugundulika
kuwa aliingiliwa kimapenzi na
kumsababishia michubuko sehemu za siri.
HISTORIA YA MLALAMIKAJI
Mlalamikaji ni kati ya watoto mapacha
waliozaliwa jijini Mwanza na mama
ambaye jina lake halikupatikana mara moja .
Mama wa mtoto huyo ( kwa sasa ni
marehemu pamoja na mume wake ) akiwa
muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies
of God ( EAGT) aliamua kumtoa mtoto
mmoja kwa mama mzazi wa Flora Mbasha
kwa lengo la kumlea, wakati huo mtoto
huyo alikuwa na miezi mitatu .
Ikaelezwa kuwa , mama wa Flora alikaa na
mtoto huyo akimsomesha hadi alipofika
darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa
Flora na kuishi naye hadi alipofikwa na
janga hilo.
Maelezo zaidi yanasema Mbasha aliweza
kufanya kitendo hicho kwa sababu mkewe
( Flora ) ameondoka nyumbani na kwenda
kuishi hotelini kwa kile kilichodaiwa kwamba
kuna ugomvi mkubwa ndani ya ndoa yao.
Taarifa zaidi zinadai kwa sasa Mbasha
naye hayupo nyumbani kwake huku
mlalamikaji yuko Hospitali ya Amana
akiendelea kufanyiwa uchunguzi wa kiafya
ili kubaini kama ana maambukizi ya
magonjwa ya zinaa au la!
Wanandoa hao katika pozi.
Kwa upande wake mlalamikaji huyo
alipopigiwa simu juzi kwa lengo la
kuthibitisha kuhusiana na sakata hilo alikiri
na kusema amekwishatoa taarifa polisi
kwa kitendo alichofanyiwa na mwenye
nyumba huyo huyo. 

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item