Mtoto wa 50 Cent alieamuakumchana baba kwa kutotokeakwenye graduation yake
Japo ni mara nyingi watoto wa kiume wameonekana kuwa na mapenzi zaidi kwa mama zao kuliko baba, haimaanishi kwamba hawamuhitaji baba k...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/mtoto-wa-50-cent-alieamua-kumchana-baba.html
Japo ni mara nyingi watoto wa kiume wameonekana kuwa na mapenzi zaidi kwa mama zao kuliko baba, haimaanishi kwamba hawamuhitaji baba kabisa kwenye maisha yao. Mtoto wa 50 Cent aitwae Marquise Jackson alitegemea baba yake ambae ni 50 Cent angehudhuria graduation yake akiambatana na watu wengine wa karibu na familia ila haikua hivyo.
50 Cent hakutokea ndio maana mwanae huyu
alipata hasira mpaka kuzionyesha kwenye mtandao wa kijamii kwa kusema ‘nilitarajia
kumuona baba yangu kwenye graduation yangu leo ila hajatokea, mama yangu na dada yangu
siku zote wako na mimi… hata hivyo nimefanikisha bila wewe’ Hata hivyo baadhi ya wanafamilia wa Marquise wanasema hii post sio ya ukweli lakini wakati huohuo wengine wanasema imeandikwa na
Marquise mwenyewe. Baadae taarifa zilitoka kwamba 50 Cent anasema hakupewa taarifa siku ya graduation ni lini na vilevile nyingine zinasema alikatazwa kuhudhuria na Mama Marquise.
50 Cent asubuhi ya May 21 2014 kwenye instagram yake zimepatikana picha mbili ambazo zinaonekana zina maneno yanayohusu hii ishu yake na mtoto. Stori kama hizi ni halali yako zisikupite…. ili niwe nakutumia kila kinachonifikia ungana na mimi kwenye twitter kwa kubonyeza HAPA , kama upo Facebook na Instagram pia unaweza kubonyeza FB na INSTA ili kupata kila stori inayonifikia zikiwemo videoz, vituko, pichaz, music na mengine yote.

