DISQUS SHORTNAME

MREMBO ANASWA KAVAA NGUOZA KUAMBIANA

AMA kweli duniani kuna sarakasi! Takribani siku kumi tangu alipofariki dunia aliyekuwa ‘ kichwa’ kwenye filamu za Kibongo, Adam Phillip Kua...


AMA kweli duniani kuna sarakasi! Takribani siku kumi tangu alipofariki dunia aliyekuwa ‘ kichwa’ kwenye filamu za Kibongo, Adam Phillip Kuambiana ( 38) , mrembo aliyejitambulisha kwa jina Mary Njombe amenaswa na nguo za staa huyo wakati mali za marehemu hazijagawanywa . Mary Njombe aliyenaswa akiwa amevaa nguo za marehemu Adam Phillip Kuambiana . Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary ambaye ni mkazi wa Magomeni Hospitali , Dar amekuwa akipigilia pamba za marehemu
hasa baada ya jamaa huyo kutangulia mbele ya haki . “Jamani njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu Kuambiana , ” kilisema chanzo chetu . Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo , wanahabari wetu walifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary . Katika mahojiano  Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho amfulie Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa akimbembeleza kuwa naye . “Mwaka 2008 ndiyo tulianza rasmi uhusiano
kwani mimi nilikuwa sina mwanaume na yeye hakuwa na mtu hivyo tulikubaliana na alikuwa akijulikana nyumbani kwetu , ” alifunguka Mary . Mwanadada huyo alisema kuwa yeye na Kuambiana walikuwa wakikutana kwenye Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni , Dar na mara nyingi alikuwa akimpikia chakula na
kumpelekea ‘ lokesheni’ .
“Nimeumia sana na sijielewi, Kuambiana ameniachia donda kubwa , nakumbuka neno la mwisho aliniambia nimpende sana kwani ipo siku nitamkubuka ,” alisema Mary huku akiangua kilio. Adam Phillip Kuambiana enzi za uhai wake akiwa amevaa shati alilonaswa nalo mrembo. Alipoulizwa kama kweli nguo hizo ni za marehemu Kuambiana , alizama ndani akatoka akiwa amevaa pensi na shati la
Kuambiana alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 17, mwaka huu baada ya kuanguka
chooni kutokana na kusumbuliwa vidinda vya tumbo.

Related

HABARI YA MJINI 843099157062007218

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item