DISQUS SHORTNAME

Master J aeleza kwanini haiwezekani ma producer wa Bongo kufanikiwa kama wasanii na kwanini alistaafu

Producer mkongwe wa muziki nchini na CEO wa  MJ Records, Master J, amesema ni ndoto kwa watayarishaji wa muziki nchini kufanikiwa kama i...


Producer mkongwe wa muziki nchini na CEO wa  MJ Records, Master J, amesema ni ndoto kwa
watayarishaji wa muziki nchini kufanikiwa kama ilivyo kwa wasanii wanaowatengenezea nyimbo.
Akiongea na Bongo5, Master J amesema hilo ndilo lililomfanya aache kutengeneza muziki na kuingia
kwenye biashara zaidi. Amesema sababu kubwa iliyotengeneza hali hiyo ni maproducer wa
Tanzania kutokuwa na umoja ambao ungewafanya kuwa na msimamo unaofanana, bei  sawa za kurekodia na utaratibu ambao ungewezesha wanufainike na matumizi ya nyimbo wanazotayarisha.
Ameeleza kuwa mara nyingi uhusiano kati ya  producer na msanii huharibika pale ambapo wimbo unapomuingizia fedha nyingi msanii kupitia show, matangazo ama ringtone wakati aliyeutengeneza akiendelea kuwa na maisha magumu.  “Unakubali pale mwanzoni lakini mwisho wa siku unakuja kugundua producer nimenyanyuliwa na mtu kama Diamond mpaka hapa sasa najulikana na sifa zote lakini huna gari, huna uwezo wa kuvaa nguo nzuri, huna hela ya kuishi sehemu nzuri, kwahiyo mwisho wa siku unakuwa mtu wa kuchekwa tu. Ndio hapo producer roho huanza  kumuuma anaanza kugombana na msanii,” amesema Jay. “Ndio maana hata mimi nikastaafu, mimi mwisho wa siku nilikuwa nataka watoto wangu wasome kwenye shule fulani, waende kwenye university fulani, nikaona hicho kitu nikaona nikiendelea hivi sitaweza kufanikisha hayo kwa kupitia muziki.
Ndio maana nikachukua hela yangu ile Mungu alinijalia kwenye muziki nikawekeza kwenye biashara nyingine, bahati nzuri namshukuru mwenyezi Mungu alinipa akili ya kufanya
biashara.”

Related

BONGO FLAVA 2107597569325182317

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item