DISQUS SHORTNAME

Marekani kutafuta mateka Nigeria

Marekani kusaidia kuwasaka wasichana  waliotekwa na Boko Haram  Marekani imesema inapeleka vifaa vya uchunguzi nchini Nigeria kusaidia ka...


Marekani kusaidia kuwasaka wasichana  waliotekwa na Boko Haram  Marekani imesema inapeleka vifaa vya uchunguzi nchini Nigeria kusaidia katika juhudi za kuwatafuta wasichana wanaozuiliwa na kundi
la Boko Haram. Wasichana hao walitekwa nyara kutoka shule  moja Kusini mwa eneo la Borno mwezi mmoja uliopita.  Msemaji wa Rais Obama Jay Carney amesema  kikosi cha maafisa 30 kiko nchini Nigeria tayari kushiriki juhudi hizo.  Amesema msaada huo wa Marekani kutoka  wizara za mambo ya nje na ulinzi na pia kutoka idara ya uchunguzi ya FBI. 
Hatua hiyo imechukuliwa wakati baadhi ya  Jamaa za wasichana waliotekwa nyara wakielezea majonzi baada ya kutazama kanda ya video iliyotolewa na kundi hilo. Marekani kusaidia kuwasaka wasichana  waliotekwa na Boko Hara Baadhi wameiambia BBC kuwa kanda hiyo imewapa matumaini lakini wameshangaa kuona wasichana hao ambao wengi ni Wakristu wamevalia mavazi ya Kiislam.  Akizungumza kwa uchungu nduguye mmoja wa  wasicha waliotekwa ameiambia BBC ni heri kanda hiyo ingeonyesha maiti za wasichana hao kwa kuwa hiyo ingeondoa wasiwasi unaoendelea kukithiri na kuumiza mioyo ya wengi. Kwenye kanda hiyo ya video kiongozi wa Boko Haram , Abubakar Shekau anasikika akiambia serikali ya Nigeria yuko tayari kubadilishana baadhi ya wasichana hao na wafuasi wake waliofungwa jela. Hatahivyo wizara ya mambo ya ndani ya Nigeria imetupilia mbali pendekezo hilo.  Seneta Ali Ndume kutoka eneo ambapo wasichana hao walitekwa nyara anaisihi serikali kulegeza msimamo.

Related

KWINGINEKO DUNIANI 803249404968142883

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item