DISQUS SHORTNAME

Loliondo kwa headline tena,sasahivi sio kikombe cha babu ni Dhahabu.

Nimeambiwa kuwa kwa sasa kuna watu wa  nguvu kibao wanaenda Samunge,Loliondo na kinachowapeleka sio ishu ya Kikombe cha babu  tena sasa h...


Nimeambiwa kuwa kwa sasa kuna watu wa  nguvu kibao wanaenda Samunge,Loliondo na kinachowapeleka sio ishu ya Kikombe cha babu  tena sasa hivi ni madini ya dhahabu ambayo  inasemekana yamegundulika eneo hilo. Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema kuwa  watu wanaongezeka kijijini hapo kwa ajili ya kujipatia madini hayo yanayosemekana yapo  katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo
za Mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na kwa Babu.
Diwani wa Samunge Jackson Sandea amesema kwa sasa kuna zaidi ya watu 4,000 na bado wanaongezeka na kusema kuwa idadi hiyo ya watu inaweza kuwa zaidi ya kikombe cha babu kwa kipindi kile. Ingawa eneo rasmi zaidi bado halijatjwa ila
inasemakana mbali na kupatikana kwenye mto  huo pia dhahabu hiyo ianapatikana hata  kwenye mashamba ya watu,kwa sasa Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini Alex Magayane amesema wanajiandaa kwenda kijijini hapo baada ya kupokea taarifa za  kugundulika kwa dhahabu kwenye eneo la
Samunge. Imeandikwa na gazeti la Mwananchi.

Related

HABARI YA MJINI 1576346464946900661

Post a Comment

  1. Hiyo samunge yenye dhahabu iko mbulumbulu karatu.na sio loliondo kama unavyosema. Fanya uchunguzi ndo uandike habari za kishamba.

    ReplyDelete
  2. Hiyo samunge yenye dhahabu iko mbulumbulu karatu.na sio loliondo kama unavyosema. Fanya uchunguzi ndo uandike habari za kishamba.

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item