KILICHOMUUA ADAM KUAMBIANA
KWELI kifo hakina huruma! Msemo huu umetimia juzi kufuatia kifo cha ghafla cha mwigizaji na mwongozaji wa filamu za Kibongo, Adam Philip ...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/kilichomuua-adam-kuambiana.html
KWELI kifo hakina huruma! Msemo huu
umetimia juzi kufuatia kifo cha ghafla cha
mwigizaji na mwongozaji wa filamu za
Kibongo, Adam Philip Kuambiana ( 38)
kilichotokea akiwa njiani kukimbizwa kwenye
Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
Mwili wa Adam Kuambiana ukipelekwa
Hospitali ya Muhimbili.
Kuambiana aliugua ghafla kwenye kambi ya
kurekodi filamu na wasanii wenzake iliyopo
katika Nyumba ya Kulala Wageni ya
Silvarado iliyopo Sinza ya Kwaremmy, Dar .
NINI CHANZO CHA KIFO ?
Akizungumza na Ijumaa Wikienda Jumamosi
iliyopita nje ya Hospitali ya Mama Ngoma,
msanii wa Bongo Fleva , Aboubakar Katwila
‘ Q- Chillah ’ alisema muda mchache kabla ya
kufikwa na mauti, Kuambiana alimlalamikia
maumivu ya tumbo ambapo Ijumaa iliyopita
alisema hali yake si nzuri kwani alikuwa
akiendesha damu tupu.
Mmoja wa wasanii aliyekuwa katika harakati
za kushuti video na Adam Kuambiana akilia
kwa uchungu .
Q- Chillah alisema : “Jana ( Ijumaa ) jioni
Kuambiana na wasanii wenzake walikuwa
baa wakinywa pombe hadi usiku mnene lakini
bado aliendelea kulalamikia maumivu ya
tumbo.
“Wenzake walimuuliza ni kwa nini alikuwa
akiendelea kunywa pombe kama anaumwa ?
Akawaambia wamuache!
“Baada ya kumaliza kunywa kila mmoja
alikwenda kulala chumbani kwake huku
tukiahidiana kwamba itakapofika saa 3: 00
asubuhi tuwe tayari kwa ajili ya kwenda
‘ location ’ .
“Lakini ulipofika muda huo sisi tukiwa tayari
kwa safari tulikwenda kugonga mlango wa
chumba chake bila mafanikio .
Yobunesh Batuli akiwa na simanzi nzito .
“Cha kushangaza, alisikika sauti yake kwa
mbali. Kwa bahati nzuri mlango ulikuwa wazi ,
mmoja akaingia ndani na kumkuta
ameanguka chooni na hajiwezi. Neno lake la
mwisho alisema kwamba anajisikia kuishiwa
nguvu na anaharisha damu .
“Kutokana na hali yake hiyo mbaya tulimbeba
na kumlaza kitandani kisha tukatafuta gari
na kumkimbiza Hospitali ya Mama Ngoma
ambapo daktari alisema kwamba alishafariki
dunia muda mrefu. ”
Rais wa Bongo Muvi , Steve Nyerere
( katikati) na Mtitu wakiwa katika hali ya
majonzi.
VIDONDA VYA TUMBO VYATAJWA
Kwa mujibu wa watu wa karibu , Kuambiana
kwa muda mrefu amekuwa akisumbuliwa na
ugonjwa wa vidonda vya tumbo ( ulcers ) .
Lakini pia inadaiwa alikuwa akisumbuliwa na
kisukari ( diabetes ) .
DAKTARI AELEZEA
Ijumaa Wikienda lilimtafuta daktari mmoja
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ( aliomba jina
kuhifadhiwa) ili azungumzie kuhusu vidonda
vya tumbo , alisema :
“Kwa kawaida , mtu kuharisha damu kwa
sababu ya vidonda vya tumbo inawezekana
kabisa , hiyo kitaalam inaitwa heamatemesis.
Inatokana na perforation ya tumbo yaani
kidonda kuwa kikubwa.
“Kwa mtumiaji wa pombe ni kipindi
anatakiwa kusimama au kuacha moja kwa
moja. Kama hatajali afya yake anaweza kufa
ghafla kwani uwezekano wa utumbo kukatika
ghafla ni mkubwa .”
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya ,
Aboubakar Katwila ‘ Q- Chillah’ na msanii
aliyekuwa akishuti video pamoja na
Kuambiana muda mfupi kabla ya kifo
wakiwa katika majonzi.
ALIJUA KIFO CHAKE
Q- Chilla ambaye ni miongoni wa wasanii
wanaocheza filamu hiyo , aliendelea kusema
kuwa siku chache kabla ya kifo, Kuambiana
alimwambia filamu yake hiyo inayoitwa Jojo
ndiyo ya mwisho , hatajishughulisha tena na
sanaa na alikuwa na mpango wa kwenda
China kupumzika kwa muda mrefu .
Ni simanzi na majonzi.
“Nimeumia sana kwani hii filamu ndiyo
ilikuwa apate fedha nyingi sana kwa sababu
ni ya kwake mwenyewe na ni kali mno ,
amecheza vizuri akinishirikisha mimi .
“Lakini ndiyo hivyo tena imeishia katikati ,
sijui ni nani atakayeiendeleza maana
mwenyewe katuachia majonzi
yasiyoelezeka, ”alisema Q -Chillah .
AMEMFUATA MDOGO WAKE
Habari zaidi zinasema kwamba, Kuambiana
ameaga dunia hata arobaini ya mdogo wake
wa damu , Patrick haijafika. Patrick alifariki
dunia mwezi mmoja uliopita .
AKUTANA NA MHARIRI WA GLOBAL
Ijumaa saa 10: 00 jioni maeneo ya Sinza
Kwaremmy jirani na Silvarado, Kuambiana
alikutana na Mhariri Kiongozi wa Magazeti
Pendwa ya Global Publishers, Oscar Ndauka .
Mhariri huyo alimuuliza ni kwa nini
hawaonani siku hizi , Kuambiana akajibu:
“Nipo Mr Ndauka , nipo bwana. Tutaonana
lakini sina hakika sana .” Kuambiana
alionekana mwenye afya njema na alimtania
mhariri huyo kwa kumwambia : “Naona siku
hizi Ndauka unazidi kunenepa tu , mi maisha
yananipiga. ”
Msanii Sandra akilia kwa uchungu .
STEVE NYERERE , BATULI WALIA SANA
Baada ya taarifa kuenea , wasanii mbalimbali
wa filamu walikusanyika katika Hospitali ya
Mama Ngoma ambapo Mwenyekiti wa Bongo
Movie Unity , Steven Mengere ‘ Steve Nyerere ’
na Yobnesh Yusuf ‘ Batuli’ walivunja rekodi ya
kulia kufuatia kifo hicho.
WADAU WAZUNGUMZIA MTU KUANGUKA
CHOONI
Wadau na mashabiki wa filamu waliokuwa
eneo hilo walisikika wakisema kwamba
wasanii wengi hawana tabia za kucheki afya
zao, jambo ambalo linawagharimu kiasi cha
kupoteza maisha.
Wengine walisikika wakisema kwamba watu
wanaoanguka chooni mara nyingi huwa
hawaponi, wakipona huwa wanapooza miili .
Mke wa marehemu Adam Kuambiana , Janeth
Rithe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kunduchi
akifarijiwa.
“Unajua watu wengi wanakosea , pale mtu
anapodondoka chooni wanamkimbiza
hospitali badala ya kumtibu kienyeji , mtu
akianguka chooni tu anatakiwa kupewa ndizi
mbivu lakini akipelekwa hospitali lazima afe, ”
walisikika watu .
HISTORIA YAKE KWA UFUPI
Marehemu Kuambiana alizaliwa mwaka 1976 ,
Ifunda mkoani Iringa. Kabila ni Mmakua wa
mkoani Mtwara.
Marehemu Kuambiana anatarajiwa kuzikwa
kesho kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini
Dar .
Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amin

Inasikitisha sana sema kaz ya mungu haina makosa!
ReplyDeleteinasikitisha mnoo. ila hapo kny kuanguka choon n ndizi mbivu bado nna ???? so kila m2 akitereza chooni ale ndizi mbivu. hatari sn hii, Mungu amlaze pema peponi
ReplyDelete