DISQUS SHORTNAME

huyu ndiye nabii waTanzania anayeponya ugonjwawa Dengue kwa Juice.

Baada ya time ya Babu wa Loliondo kuponya kwa kutumia kikombe,sasa ni time ya kiongozi wa dini ambaye anajiita nabii na kutangaza kuwa an...


Baada ya time ya Babu wa Loliondo kuponya kwa kutumia kikombe,sasa ni time ya kiongozi wa dini ambaye anajiita nabii na kutangaza kuwa anatibu ugonjwa wa Dengue kwa kutumia juisi.
 Nabii huyu anayejulikana kwa jina la Yaspi Bendera baada ya taarifa zake kusambaa kumefanya baadhi ya wagonjwa kuanza kwenda kwenye kanisa lake la Ufunuo kwa Watu Wote lililopo Yombo Buza-Kipera. Ingawa Serikali imeonya vitendo vya baadhi ya watu kuwaondoa wagonjwa hospitalini na kuwapeleka kwenye maombi na kusema mtu yeyote anayesababisha wagonjwa kuondolewa hospitalini kwenda kufanyiwa maombi atachukuliwa kuwa ni adui namba moja,katika jitihada za kupambana na ugonjwa huo na
kusisitiza kuwa wagonjwa ni lazima kwanza watimize dozi wanazopewa na wataalamu hospitalini ndipo waendelee na imani zao. Taarifa ya wataalam inasema kuwa ugonjwa huo unatokana na mbu aina ya aedes Egypt sasa Nabii Yaspi anadai kuwa homa ya dengue ni pigo lililoletwa na Mungu kwa watu wasiotaka kumtii.Nabii huyo anadai kuwa alionyeshwa na Mungu miezi miwili iliyopita kuwa homa ya ugonjwa huo ingeibuka nchini na kwamba itawaathiri zaidi watu wazima kuliko watoto.Nambii huyo kasema kuwa moyoni ana siri nzito ambayo atamwambia mkuu wa nchi peke yake ambaye ni Rais Jakaya Kikwete na endapo atakosa nafasi ya kufanya hivyo hatamwambia mtu mwingine.

Related

STORY ZA KITAA 5892117918837131038

Post a Comment

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item