DISQUS SHORTNAME

GLOBAL WAMPA ZA CHEMBE LULU

LULU NI UTOTO TU , AKIKUA  ATAACHA NADHANI ndicho kitu pekee ninachoweza  kusema , ili kuweza kwenda sawa na muigizaji  Elizabeth Michae...

LULU NI UTOTO TU , AKIKUA  ATAACHA
NADHANI ndicho kitu pekee ninachoweza  kusema , ili kuweza kwenda sawa na muigizaji  Elizabeth Michael , ambaye mashabiki wake wanamfahamu zaidi kama Lulu . Kwamba  binti huyu mwenye umri wa miaka 19 sasa , anasumbuliwa na utoto ambao bila shaka  akishapevuka, ataachana nao ! Niwe mkweli, sijawahi kukutana na binti huyu, iwe kikazi au kwa bahati mbaya .  Nimekuwa nikimsikia tu , ingawa kwa nature ya kazi yangu, nafuatilia kwa karibu sana  nyendo zake , hasa zinazohusiana na kazi  yake ya kisanii . Mimi ni mdau wa filamu , nimeanza kuangalia  kazi zao tokea zilipoanza miaka ile ya 2000 ( filamu za kizazi kipya ) . Nimekuwa nikisema  mara kwa mara na wala sioni aibu kurudia ,  sinema zinazotengenezwa na wasanii wetu zipo chini mno ya kiwango , ingawa baadhi ya  wasanii wachache wana uwezo na vipaji vyao
binafsi. Filamu zetu hazishawishi. Ingawa wote  tunajua kuwa ni maigizo, lakini yamezidi mno  kiasi kwamba unapata tabu unapokutana na muigizaji wetu akikuambia sasa anataka  kusaka soko la kimataifa.
Sina uhakika soko la kimataifa maana yake ni nini, kwamba  kuuza kazi zao nje ya Tanzania , kwa maana
ya Kenya , Uganda , Rwanda, Burundi , DRC , Malawi na nchi nyingine Afrika au  wanamaanisha nje ya Afrika . Kama nilivyosema hapo awali , sijawahi  kuonana na Lulu, lakini mbaya zaidi , sijawahi
kuona filamu yake yoyote, kiasi ambacho nitakuwa mwongo nikisema anajua au hajui  kuigiza . Ila kilichonifanya niseme naye kupitia safu hii , ni kauli yake ya wiki iliyopita wakati  alipozungumza na moja ya magazeti ya  Global Publishers . Alikuwa akiomba mamlaka zinazohusika na  maadili ya filamu , kuacha kuwabana sana wasanii kuhusiana na mavazi, kwani endapo  wataruhusiwa kuigiza wakiwa nusu utupu,
itawasaidia katika soko la kimataifa. Hapa ndipo nilipo na mashaka na akili ya  muigizaji huyu, kwani kwa uelewa wa kawaida kabisa , ili kazi zao ziweze  kununuliwa kwa wingi huko anakokuita  kimataifa, ni lazima watu waone vitovu, mapaja , matiti na huenda hata makalio ya waigizaji wetu !  Moja ya sababu zinazofanya filamu zetu kukosa ubora, ni akili za waigizaji wenyewe  wa aina ya akina Lulu . Kinachofanya watu
wanunue na kupenda kazi za wasanii ni ubunifu wao katika kazi husika na wala siyo  mavazi au pozi zao.
Enzi sisi tunakua, tulikuwa tukiangalia sana filamu za Kihindi katika majumba ya sinema.  Ingawa Wahindi wameendelea kulinganisha na sisi , lakini filamu zao hazikuruhusu  uzungu kabisa , waigizaji walicheza muziki  ( wa kwao ) , walishikana na hata kubusiana kwa nidhamu ya hali ya juu na wala waigizaji  wao wa kike hawakuwahi kuonekana katika mavazi ya nusu utupu !  Tazama sasa , pamoja na kuwa hatukujua
Kihindi, lakini mpangilio mzuri wa stori, ulitufanya tuelewe kuanzia mwanzo hadi  mwisho juu ya kitu gani wahusika walitaka kukituma kwetu kama walaji . Ndiyo maana  kulikuwa na mashabiki wengi sana nchini wa
waigizaji kama akina Amitab Bachchan , Mithun Chakraborty , Amjad Khan , Shashi  Kapoor na wengineo wengi wa enzi hizo   Hivi sasa ukiangalia filamu zetu,  zilizotengenezwa kwa lugha yetu , mtu huelewi
nini hasa waswahili wenzetu hawa walikusudia kutuambia. Kumbe hawajui  namna ya kutushika kwa sababu akili zao zinawaza jinsi gani tunavyokoma na maumbo  yao!  Kitakachofanya wauze wala siyo uvaaji hata kidogo. Ninaamini kabisa hata akina Lulu leo waruhusiwe kuigiza wakiwa watupu kabisa ,  sidhani kama wanaweza kutuletea kazi ya maana zaidi tu ya kuonekana vituko huko  kimataifa wanakotaka .  Waigizaji wetu wana soko kubwa sana la kazi yao katika nchi za Afrika Mashariki na Kati kama wataboresha uigizaji wao , kutuwekea vitu vinavyoendana na uhalisia wa wanachotaka kutuletea lakini siyo kuamini  katika maumbo ya miili yao. Ndiyo maana nikatilia shaka hilo soko lao la  kimataifa wanaloamini kwa nusu utupu,
huenda sikumuelewa. Labda ana maana nyingine ambayo mimi na wewe hatuelewi .

Related

INAHU 9185347223458799187

Post a Comment

  1. Heehehe ila kweli siamin kama kuvaa uchi kutasababisha soko la filam kupanda mfano mzuri hata hao wazungu wenyewe movie zao nyingi hawavai uchi ila zinapendwa sana mfano wa movie my last day without you and temptation ni movie zilizofanikiwa ila washiriki hawakuacha maungo yao wazi ili kuuza movie I think huo ni ulimbuken tu wa kuonesha viungo vyao vya mwili ambavyo pia sio maadili me naona wanawake wa kitanzania wanapenda kujidhalilisha wenyewe kwa kweli.

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item