DISQUS SHORTNAME

DIAMOND AENDA KULALA KWA WEMA NA TUZO ZAKE 7 ...NDUNGU WAMINDI

ZILE tuzo saba alizotwaa nyota wa Bongo Fleva , Nasibu Abdul ‘ Diamond ’ kwenye mkesha wa Jumapili iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mlimani Ci...

ZILE tuzo saba alizotwaa nyota wa Bongo Fleva , Nasibu Abdul ‘ Diamond ’ kwenye mkesha wa Jumapili iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam zimezua balaa ! Ni balaa gani hilo? Risasi Jumatano linakumegea. Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu  Kwa mujibu wa chanzo makini, baadhi ya ndugu wa Diamond walicharuka kufuatia staa huyo aliyeshinda nafasi ya Msanii Bora wa Kiume wa Bongo Fleva 2014 , kuzibeba tuzo hizo na kwenda kulala nazo kwa Wema Sepetu anayemtaja kuwa ni mpenzi wake kwa sasa .
MANENOMANENO YA BAADHI YA NDUGU
“Unajua kilichowakwaza sana baadhi ya ndugu ni kitendo cha Diamond kwenda kulala
kwa Wema , Kijitonyama na tuzo zote saba. “Wanasema alichotakiwa kukifanya , mara
baada ya kutoka ukumbini angekwenda nazo nyumbani kwao ( Sinza - Mori) akaziacha kisha
ndiyo aende kwa huyo Wema wake, ” kilisema chanzo hicho. Kikaongeza: “Ujue Diamond anakoelekea anaanza kupotoka kwani mwanzo alikuwa haachani na mama yake hasa kwenye ishu kubwa kama hizo , mwaka huu ameonesha utovu wa nidhamu , maana ndugu wanaamini hakutaka kwenda na mama yake ukumbini kwa sababu alijua atakuwa na Wema .”

MARAFIKI PIA WASHANGAZWA
Chanzo kiliendelea kuanika kwamba baadhi ya marafiki wa Diamond nao walionesha
kushangazwa na kitendo cha mama Diamond  ( Sanura Kasim ) kutoonekana kwenye ukumbi
wakati mwanaye akipokea tuzo badala yake nyota huyo kuwa beneti na Wema . Diamond akipokea tuzo kutoka kwa prodyuza Tuddy Thomas . “Baadhi ya marafiki wamesema kuna kitu , kwa vile wanavyojua wao , shoo au jambo lolote ambalo Diamond anahusika, mama yake lazima aibuke naye . Wengi wanaamini uhusiano wa mama na mwanaye umevurugwa na kitendo cha Wema kurudiana na baby wake huyo, ” kilisema chanzo hicho. Kikaendelea : “Lakini kuna watu wanadai mama Diamond siku hiyo aliamua kwenda kwenye bethidei ya mpenzi wa zamani wa Diamond , yule Penny kwa sababu alipuuza uwepo wa Wema ukumbini .”
NDUGU WASAKWA
Baada ya paparazi wetu kuzinyaka taarifa hizo , alianza kuwasaka baadhi ya ndugu hao
ili kujua ukweli wa madai yote.
WA KWANZA MAMA DIAMOND
Mtu wa kwanza kupatikana kwenye familia hiyo ni mama Diamond mwenyewe ambapo alibanwa kwa maswali kadhaa kama ifuatavyo :
Paparazi: “Mama Nasibu nimekuja kwa mambo mawili matatu. Kwanza nataka kujua ni kwa nini hukuonekana ukumbini siku ya Tuzo za Kili wakati mwanao anazoa tuzo saba? Maana wengine wanasema uliogopa uwepo wa Timu Wema , wengine wanasema ulikwenda kwenye bethidei ya Penny.
Penny akiwa katika pozi. Pia kuna minong ’ ono kwamba, familia imechukizwa na kitendo cha Diamond kwenda kulala na tuzo zake nyumbani kwa Wema , ni kweli ?
Mama: “Kwanza kabisa , siku ile mimi sikuwa na mpango wa kwenda kwenye shughuli hiyo , hasa niliposikia itaoneshwa laivu kwenye runinga. “Napenda kukwambia kwamba kuanzia sasa huo ndiyo utakuwa utaratibu wangu. Zamani nilikuwa nikienda kwenye shoo, hasa zinazomuhusisha Diamond kwa vile nilikuwa sijamuona namna ya utendaji kazi wake lakini sasa namwamini anaweza kuchapa kazi hata mimi nisipokuwepo .
. .. akipozi na mpenzi wake wema Sepetu .
KUHUSU TIMU WEMA , BETHIDEI YA PENNY
“Wanaosema mimi sijaenda ukumbini kwa sababu eti nilikuwa nikihofia Timu Wema si kweli na wala sikwenda kwenye bethidei ya Penny kama wasemavyo .
“Ninaomba itambulike kwamba mimi siko kwenye timu yoyote ile , kama timu basi mimi nipo Wasafi ( ya Diamond ) kwa maana ninamsapoti mwanangu kwa kila kazi yake na wala sina kitu tofauti na hicho. ”
DIAMOND SASA
Diamond naye alikutwa nyumbani kwao siku hiyo akiwa na tuzo hizo ambazo ilidaiwa alikwenda nazo asubuhi iliyofuata baada ya kuamka kwa Wema , alipoulizwa juu ya kupitiliza nazo hadi nyumbani kwa Wema badala ya kuzipeleka kwa mama yake , alionekana kushindwa kujibu zaidi ya kucheka na kusema :
“Wabongo bwana, hawakosi sababu na maneno ya kuongea kwa kila kitu hata kama ningefanya nini lazima wangepata tu kipya cha kunizungmzia hivyo kwa hilo sina hata cha kujibu ila tuzo zipo hapa nyumbani kwa
mama.”
KUHUSU MAMA YAKE KUTOKWENDA UKUMBINI
“Kuhusu mama kutokwenda ukumbini mimi najua wazi kwamba hakuhitaji na aliomba aangalizie nyumbani kupitia runinga na kusema kweli nimefurahi sana kupata tuzo hizi ingawa pia furaha yangu itakuwa kubwa
sana kama nitanyakua na tuzo ya Channel O , ” alisema Diamond .
HALIMA KIMWANA
Baada ya Diamond kuweka wazi, paparazi wetu alimtafuta Halima Kimwana ambaye naye alidaiwa kukacha kuzama ukumbini hapo kwa kuwa tu hana uhusiano mzuri na Wema na kwamba siku hiyo anadaiwa
kwenda kwenye bethidei ya Penny ambaye ndiye rafiki yake kipenzi kwa sasa tangu alipoachika kwenye penzi la Diamond , msikilize Halima :
“Jumamosi siku tuzo zinatolewa mimi nilikuwa safarini Morogoro ambapo nilikwenda kufanya mambo yangu na mjini nilirudi Jumapili na mchana huohuo nilikwenda kweli kwenye bethidei ya Penny . “Naomba ieleweke kwamba mimi sijakimbia timu yoyote na wala sitambui kama kuna kitu kinaitwa Timu Wema ila najua tu kaka Diamond ana uhusiano na Wema Sepetu , sijui hiyo Timu Wema ndiyo chombo gani ?
Credit by:global publisher news

Related

BONGO FLAVA 7770347797438441536

Post a Comment

  1. Aaaaaa nimempenda mama Eti akipoz namempenzi wake Wema naeee alima ameamua kujilipuaa duuuuuh ninachojua diamond Yuko nampenzi wake Wema duuuuuh ni raha tuuuu

    ReplyDelete
  2. Wataelewa tu taratibu

    ReplyDelete
  3. SI WAMEZOEA USWAHILI WATAWEZAJE KUKAA NA MZUNGU WA SURA NA ROHO........

    ReplyDelete
    Replies
    1. Familia za kiswahili zina tabu sana hata uzipe maisha bora uswahilibutabaki kua palepale money cnt buy class neither civilisation.Mama Diamond bariki furaha ya mwanao na fungua moyo kujifunga kwa roho yako na kusononeka utakua unamzibia mwanao neema zisizo onekana. Diamond m2 mzima sio mtoto wa miaka 10 mumpangie la kufanya.kwanza huoni furaha mwaka jana mwanao alitoka na tuzo moja alipo kua na oenny leo karudi kwa furaha yake zimemwagika 7 nyota yake ing'aa zaidi hapo jwa sepetu na mama yake mzazi sandra unatambua hilo pia hao ma wifi.Msilete chuki zilizotanda na wivu zikamrudisha nyuma kama kweli mnapenda huyo Nasibu. Mama Diamond kwa muonekano unaonekana mama mshkaji basi kula na mwanao sahani moja hajamzaa kimwana huyo wala hana damu nae usiingizwe kwenye mambo ya kitoto we mama unajua furaha mwanao kuliko wote asinge kua hana ki2 huyo wasinge angaika hao dada zake mbona hatukuwasikia zamani enzi za nenda kwa mwambie .Sandra mama roho ya diamond bless wat u son desire nt wat dada zake wanataka ushamba uliyo kithiri.wat jah bless no man can break

      Delete
    2. hehe u,meonaeeeh halima liswahili sana eti halijui teamwema toka hapa unaijua sana wewe mwenyewe unatumia acc fake najina lako ni nauzakundukwadolamia4 wewe halimakimwana usituzingue hapa teampenny wote nimarafiki wa penny

      Delete
    3. mbona kama maza kapiga licha na mwanae kweny same background na walopiga wemond.au mi ndo sijaelewa au mambo ya pic mix......wabongo bwana.

      Delete
  4. Diamond na Wema, Wema na Diamond. In short!!!! Mama watakie kila la heri tu. Muacheni
    daimond afanye maamuzi yake he is a grown up man now.

    ReplyDelete

Comment zako Kuhusu hii stori

emo-but-icon

Hot in week

Recent

Comments

item