Chris Brown aongezwa muda jela
Brown alifungwa jela baada ya kumchapa aliyekuwa mpenzi wake Rihana Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown atasalia jela kwa siku nyingine ...
https://mirindimoyapwani.blogspot.com/2014/05/chris-brown-aongezwa-muda-jela.html
Brown alifungwa jela baada ya kumchapa
aliyekuwa mpenzi wake Rihana
Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown atasalia
jela kwa siku nyingine 131 baada ya kukiri
kukiuka amri ya mahakama kuhusu kifungo cha
nje alichokuwa amepewa na mahakama.
Muimbaji huyo wa muziki wa mtindo wa R&B
alikiri mahakamani mjini Los Angeles mnamo siku
ya Ijumaa kuwa alitenda uhalifu mjini Washington
Oktoba mwaka jana.
Jaji alimuhukumu kifungo cha siku 365 jela
ingawa alimpongeza kwa kuhudumia siku 234
katika kituo cha kupata ushauri nasaha.
Brown amekuwa chini ya aungalizi wa mahakama
tangu mwaka 2009 alipokiri kumpiga
mwanamuziki mwenza na ambaye alikuwa
mpenzi wake wakati huo,Rihanna.
Mshindi huyo wa tuzo la Grammy amekuwa
kizuizini tangu mwezi Machi alipokamatwa kwa
kukiuka amri ya mahakama iliyomweka ndani ya
kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.
Kifungo alichopata kuongezewa siku kinahusiana
na kisa cha ugomvi kilichotokea mjini DC mwaka
jana.
Brown anakabiliwa na mashitaka ya kumchapa
mwanamume mmoja nje ya hoteli moja mjini
Washington
Source: BBC
